Ushauri kutoka kwa Naval Ravikant kupitia mtandao wa twitter @naval mwaka 2018.
Naval Ravikant ni milionea mjasiriamali na mwekezaji wa nchini marekani. Ni mwanzilishi wa kampuni ya AngelList ambayo inawaunganisha wajasiriamali na wawekezaji wakubwa. Amewekeza kwenye makampuni mbalimbali makubwa kama Facebook, Twitter na mengineyo.
Mwezi Mei mwaka 2018 kupitia mtandao wa twitter, Naval alipata msukumo wa kushirikisha kile anachojua kuhusu kufikia utajiri bila ya kutegemea bahati. Alichoshirikisha kilipata umaarufu mkubwa na kusambazwa kwa wengi na kwa njia mbalimbali.

Kwenye makala hii nakwenda kukushirikisha yale yote aliyoshauri Naval kuhusu kufikia utajiri bila ya kutegemea bahati. Karibu tujifunze misingi sahihi ya kufanyia kazi ili tuweze kufikia utajiri na uhuru wa kifedha.
Hivi ndivyo Naval anavyotushauri kuhusu kufikia utajiri bila ya kutegemea bahati;
Tafuta utajiri na siyo fedha wala hadhi.
Utajiri ni kuwa na mali zinazokuingizia kipato ukiwa umelala.
Fedha ni jinsi unavyobadili muda na utajiri.
Hadhi ni nafasi yako kwenye ngazi za kijamii.
Tambua kwamba kutengeneza utajiri halali ni kitu kinachowezekana.
Kama unaudharau utajiri kwa siri, utakukimbia.
Puuza watu wanaocheza mchezo wa hadhi.
Huwa wanajipa hadhi kwa kuwashambulia wale wanaocheza mchezo wa kujenga utajiri.
Huwezi kutajirika kwa kuwakodishia wengine muda wako.
Ni lazima umiliki mali au biashara itakayokufikisha kwenye uhuru wa kifedha.
Utatajirika kwa kuipa jamii kile ambacho inataka lakini haijui jinsi ya kukipata.
Na ufanye hivyo kwa kiwango cha juu.
Chagua tasnia ambayo unaweza kucheza mchezo wa muda mrefu na watu wa muda mrefu.
Intaneti imerahisisha na kupanua uwanja wa kazi.
Watu wengi bado hawajalijua hilo.
Cheza michezo ya kujirudia.
Marejesho yote kwenye maisha, iwe ni utajiri, mahusiano au ujuzi, huwa yanakuja kwa riba mkusanyiko.
Chagua mshirika wa biashara mwenye akili, nguvu na zaidi ya yote, mwenye uadilifu.
Usishirikiane na mwenye mtazamo hasi na aliyekata tamaa.
Maana kile wanachoamini ndiyo kinachotokea.
Jifunze kuuza.
Jifunze kujenga.
Ukiweza kufanya hivyo viwili, hakuna kitakachoweza kukuzuia.
Jijengee ujuzi mahsusi, uwajibikaji na nyenzo.
Ujuzi mahsusi ni ule ambao hakuna anayeweza kukufundisha.
Kama jamii inaweza kukufundisha kitu, basi pia inaweza kumfundisha mtu mwingine na akachukua nafasi yako.
Ujuzi mahsusi hupatikana kwa kujua kusudi lako, kile unachopenda na unachokidadisi sana badala ya kuhangaika na fursa mpya kila wakati.
Kujenga ujuzi mahsusi kwako itakuwa kama mchezo, wakati kwa wengine itakuwa ni kazi ngumu.
Ujuzi mahsusi unapofundishwa ni kupitia uanagenzi na siyo shule.
Ujuzi mahsusi mara nyingi ni wa ufundi wa hali ya juu au ubunifu.
Hauwezi kutolewa kwa wengine au kugeuzwa kuwa rahisi kutolewa.
Kumbatia uwajibikaji, na chukua hatari za kibiashara chini ya jina lako mwenyewe.
Jamii itakuzawadia majukumu, mali na nyenzo.
Watu wanaowajibika zaidi wana jina moja, ambalo liko hadharani na tayari kuchukua hatua za hatari, mfano Oprah, Trump, Kanye, Elon.
“Nipe nyenzo ndefu na mahali pa kusimama na nitaweza kuisogeza dunia.” – Archimedes.
Utajiri unahitaji nyenzo.
Nyenzo ya kibiashara inatokana na mtaji, watu na bidhaa ambayo haina gharama za ziada kwenye kuzalisha (mfano programu za kompyuta na maudhui ya kidijitali.)
Mtaji unamaanisha fedha. Kupata fedha tumia ujuzi wako mahsusi na uwajibikaji na onesha matokeo ya maamuzi mazuri.
Nguvu kazi inamaanisha watu wanaokufanyia kazi.
Ndiyo njia ya zamani na iliyozoeleka ya kupata nyenzo.
Nyenzo ya nguvu kazi itawafurahisha wazazi wako, lakini usipoteze maisha yako kuitafuta.
Mtaji na nguvu kazi ni nyenzo unazohitaji kutoka kwa wengine.
Kila mtu anatafuta mtaji, lakini unahitaji mtu wa kukupatia.
Kila mtu anakazana kuongoza, lakini unahitaji mtu wa kukufuata.
Programu za kompyuta na maudhui ya kidijitali ni nyenzo ambayo huhitaji kupata kwa wengine.
Hizi ndiyo nyenzo zilizo nyuma ya utajiri mpya.
Unaweza kutengeneza programu za kompyuta au maudhui ya kidijitali ambavyo vitakufanyia kazi ukiwa umelala.
Jeshi la maroboti liko wazi na linapatikana bure kabisa, litumie.
Kama huwezi kutengeneza programu za kompyuta basi tengeneza maudhui, andika vitabu, blogu, rekodi video au sauti.
Nyenzo ni nguvu inayozidisha maamuzi unayofanya.
Nyenzo inakuza matokeo ya maamuzi yako.
Maamuzi sahihi yanahitaji uzoefu ambao unaweza kujijengea haraka kwa kujifunza ujuzi wa msingi.
Hakuna ujuzi unaoitwa biashara.
Epuka majarida ya biashara na madarasa ya biashara.
Badala yake jifunze uchumi, saikolojia, ushawishi, maadili, hisabati na kompyuta.
Kusoma ni haraka kuliko kusikiliza.
Kufanya ni haraka kuliko kutazama.
Unapaswa kuwa ‘bize’ kiasi cha kutokuwa na muda wa kupoteza lakini pia uwe umepangilia mambo yako vizuri.
Jiwekee thamani ya fedha ya kila saa yako moja ya kazi.
Kama kutatua tatizo kunaokoa kiasi cha fedha ambacho ni kidogo kuliko thamani ya muda uliotumia achana na tatizo hilo.
Kama kumlipa mtu mwingine kusaidia jukumu itakugharimu kiasi kidogo cha fedha kuliko thamani ya muda wako, mlipe mwingine akusaidie jukumu hilo.
Fanya kazi kwa bidii kubwa uwezavyo.
Lakini pia wale unaofanya nao kazi na kile unachofanyia kazi ni muhimu kuliko bidii unayoweka kwenye kazi.
Kuwa bora kuliko wote duniani kwenye kile unachofanya.
Endelea kuboresha kile unachofanya mpaka kufikia kiwango hicho cha ubora.
Hakuna njia ya mkato ya kupata utajiri.
Ukiona mtu anakuja kwako na njia hiyo jua anataka kutajirika kupitia wewe.
Tumia ujuzi mahsusi pamoja na nyenzo na mwisho utapata kile unachostahili.
Na hatimaye unapofikia utajiri, ndiyo unagundua kwamba utajiri siyo kitu ulichokuwa unatafuta.
Lakini hilo ni somo la siku nyingine.
Karibu kwenye mazingira yatakayokuwezesha kuishi misingi hii.
Rafiki yangu mpendwa, misingi ya kufikia utajiri wa uhakika kutoka kwa Naval Ravikant inaeleweka kwa urahisi kabisa, na hakuna kitu ambacho ni kipya kabisa. Lakini katika watu 100 watakaojifunza na kuelewa misingi hii, ni 10 pekee ambao wataifanyia kazi. Na katika hao 10 watakaoifanyia kazi, ni mmoja pekee atakayeweza kufikia utajiri mkubwa kabisa.
Matokeo huwa yanakuwa hivyo kwa sababu jamii zetu zina njia mbalimbali za kuwakwamisha watu na kuwarudisha nyuma. Jamii haitakuachia kirahisi ufike kwenye utajiri mkubwa, badala yake itakuwekea vikwazo vya kila aina. Hivyo inahitaji uwe umejitoa kweli kweli ili kufikia lengo lako la utajiri.
Unahitaji kuwa kwenye mazingira sahihi, mazingira yanayokusukuma kuendelea kuishi misingi hiyo kila siku na kwa muda mrefu. Mazingira ambayo yataendelea kukukumbusha misingi hii mara kwa mara. Na pia mazingira ambayo umezungukwa na wengine wanaoishi misingi hiyo. Uzuri ni kwamba mazingira ya aina hiyo tayari yapo, ni wewe kuchukua hatua ili uweze kunufaika nayo.
Mazingira hayo ni kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, unaishi kwa msingi, mwongozo na msimamo sahihi wa mafanikio, hivyo ni vitu ambavyo unavitumia kufanya kila aina ya maamuzi yako, kitu ambacho kitakusaidia kuishi misingi hii tuliyojifunza ya kufika kwenye utajiri mkubwa.
Ndani ya KISIMA unapata nafasi ya kujua kusudi la maisha yako, kujua nini hasa unachopendelea kufanya na kwa kutumia miongozo iliyopo, utaweza kujifunza jinsi gani watu wanaweza kukulipa kwa kufanya kile unachopenda kufanya.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA unalazimika kuwa na biashara au uwekezaji ambao utakulipa baadaye hata kama hufanyi kazi moja kwa moja, kitu ambacho ni muhimu mno kwenye kufikia utajiri.
Wote tunajua kwamba mshahara huwa hauleti utajiri, bali unakuletea fedha, jinsi unavyotumia fedha hizo ndiyo unaweza kujenga utajiri au umasikini. Wengi hufikiri ukitumia mshahara kujenga nyumba ya kifahari ya kuishi na kuwa na magari ya kifahari ndiyo utajiri. Huo ni umasikini mkubwa, kwa sababu nyumba au gari lako la kifahari havitakuingizia hata senti moja siku utakayokuwa huna mshahara, zaidi vitataka fedha kutoka kwako.
Ndiyo maana kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hata kama una mshahara mkubwa kiasi gani, unapaswa kuwa na biashara au uwekezaji unaoujenga, ambao miaka ijayo utakuwa unakuzalishia wewe faida hata ukiwa umelala.
Pia kwenye KISIMA, tunaishi kwenye msingi mkuu wa kazi, kwamba kazi ndiye rafiki wa kweli, kazi ndiyo njia pekee ya kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Tunaamini kwamba hakuna chochote halali na kinachodumu utakachoweza kukipata bila ya kuweka kazi ya wazi kabisa na inayoonekana na kila mtu. Tunaishi kwa falsafa hii; unaweza kupata chochote unachotaka kama utawapa wengine kile wanachotaka.
Kikubwa ni kwamba unapokuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unachagua lengo lako kuu unalifanyia kazi na eneo unalotaka kubobea, kisha unakomaa na vitu hivyo kwa angalau muongo mmoja (miaka 10) bila ya kuhangaika na vitu vingine. Unapochagua eneo moja na kukomaa nalo, ni lazima utafikia utajiri mkubwa kama tulivyojifunza kwenye ushauri wa Naval, ambaye ametuambia tujijengee ujuzi mahsusi na kuwa bora kuliko wote duniani kwenye kile tunachofanya.
Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajizuia wewe mwenyewe kufikia utajiri mkubwa kwenye maisha yako. Unaweza kufurahia kipato unachoingiza sasa lakini ukashindwa kufanya uwekezaji sahihi na baadaye mambo yakawa magumu sana kwako.
Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili uweze kujijengea utajiri mkubwa na wa uhakika kupitia misingi utakayokwenda kuiishi kila siku ya maisha yako. Kwa utajiri utakaoweza kujijengea kutokana na mafunzo na miongozo ya KISIMA CHA MAARIFA, ni mkubwa mno ukilinganisha na ada utakayolipa ili kujiunga. Utapanda mbegu ndogo, na kama utafanyia kazi yale unayojifunza basi mavuno yake yatakushangaza sana.
Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.
KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.
KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.
Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;
1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.
2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)
3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.
5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.
6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.
7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.
8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.
9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.
10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.
Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.
Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.
Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.
Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.
Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania