“If there is something great in you, it will not appear on your first call. It will not appear and come to you easily, without any work and effort.” —RALPH WALDO EMERSON
Kila mmoja wetu ana ukuu ndani yake,
Ndiyo, hiyo inajumuisha na wewe pia.
Una uwezo mkubwa sana ndani yako,
Uwezo wa kufanya mambo makubwa na ya kipekee.
Yale makubwa unayoona wengine wanafanya na yanakuvutia,
Kuna makubwa yako pia unayoweza kufanya na yakawavutia wengi.
Kama hujaweza kufanya makubwa kwenye maisha yako,
Siyo kwa sababu huna ukuu,
Bali kwa sababu hujaweka kazi ya kutosha ndani yako ili kufikia ukuu wako.
Ukuu ulionao hauonekani kirahisi,
Hutaweza kuufikira kwa kuishi kwa mazoea kama watu wengine.
Bali utaufikia baada ya kuweka kazi hasa, kazi kwako binafsi, ya kitambua ukuu wako na kuutumia.
Kufikia ukuu wako na kuutumia unahitaji kutumia akili yako kufikiri,
Kusikiliza roho yako inakuambia nini,
Kuusukuma mwili wako kwenda zaidi ya ulivyozoea,
Na kuwa na utulivu wa hali ya juu, unaokuwezesha kujisikiliza na kuweka juhudi sahihi.
Siyo rahisi kufikia na kutumia ukuu wako,
Ndiyo maana kati ya watu 100, mmoja pekee ndiye anayefikia ukuu na mafanikio makubwa,
Huku wengine wakibaki kawaida.
Kama unataka kuwa huyo mmoja, kazi inahitajika.
Kuwa tayari kuweka kazi kwako binafsi na itaweza kufanya makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania