“Both our physical sufferings and periods of depression are part of our life in this world, and we should patiently wait until they are over, or our life is over.” – Leo Tolstoy

Hakuna mtu ambaye hapitii maumivu fulani kwenye maisha yake,
Kila mtu na kila wakati kuna maumivu fulani anakuwa anapitia,
Kuna ugumu anakuwa anapambana nao,
Kuna matatizo, changamoto na vikwazo vinamkabili.
Hivyo ndivyo maisha yalivyo, mpaka siku tunaondoka hapa duniani.

Ukiona mtu anacheka na kuwa na furaha wakati wote,
Siyo kwa sababu hana maumivu,
Bali kwa sababu amejifunza kuishi na maamuzi aliyonayo.
Hivyo na wewe usisubiri mpaka maumivu yaishe ndiyo uyafurahie maisha,
Badala yake yafurahie maisha sasa, licha ya maumivu au magumu unayopitia.

Kwa sababu kuna wengine wengi sana wangetamani kuwa hai hata kama wangekuwa na maumivu au magumu kuliko unayopitia wewe.
Chagua leo kuyaishi maisha yako kwa ukamilifu na furaha,
Usijiambie unasubiri mpaka maumivu na magumu yapite,
Kwa kuwa hata yakipita, yatakuja mengine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania