“Concentrate on what’s in front of you like a Roman. Do it like it’s the last and most important thing in your life.” – Marcus Aurelius
Wengi huanza siku zao wakiwa na mipango mbalimbali,
Wanamaliza siku hizo wakiwa wamechoka kweli kweli,
Lakini wakiangalia walichofanya, hawaoni.
Wamesumbuka siku nzima na kuchoka, lakini hakuna matokeo ya maana wanayokuwa wamezalisha.
Yote hiyo ni kwa sababu ya kukosa vipaumbele.
Unapokuwa huna kipaumbele, maana yake kila kitu kwako ni lipaumbele.
Hivyo ukiwa unafanya jambo moja na jingine likaja, utaacha unachofanya na kwenda kufanya hicho kingine.
Huna kipaumbele, hivyo ni vigumu kwako kupima.
Njia pekee ya kuondokana na hali hiyo ni kufuata ushauri wa Mstoa Marcus Aurelius,
Ambaye anatuambia kitu muhimu zaidi kwetu kufanya ni kile kilicho mbele yetu, kile tulichochagua kukifanya.
Tunapaswa kukifanya kitu hicho kama vile ndiyo kitu cha mwisho kwetu kufanya hapa duniani, kama vile ndiyo kitu muhimu kuliko vingine vyote.
Kwa sababu ni kweli ndiyo kitu muhimu zaidi, la sivyo hukupaswa hata kukifanya.
Na pia kinaweza kuwa ndiyo kitu cha mwisho kwako kufanya, maana hakuna ajuaye kesho yake.
Kitu muhimu cha kuondoka nacho kwenye tafakari hii ni hiki; weka vipaumbele na vifuate hivyo.
Hiyo ndiyo njia pekee ya kuweza kufanya makubwa hapa duniani.
Pia usiahirishe chochote na kujiambia utafanya kesho, huna uhakika ma hiyo kesho.
Unayo leo, itumie kufanya yale muhimu tu, yasiyo muhimu achana nayo, hayastahili muda wako adimu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania