“What we perceive as limitations have the potential to become strengths greater than what we had when we were ‘normal’ or unbroken…when something breaks, something greater often emerges from the cracks.” — Nnedi Okorafor

Kile unachoona kama kikwazo kwako kufika kula unakotaka kufika, ndiyo njia unayopaswa kuitumia kufika unakotaka.
Ule unaoona kama udhaifu unaokufanya ushindwe kufanya unachotaka, ndiyo uimara ambao utakuwezesha kufanya kitu hicho.

Vikwazo na udhaifu ni njia ya asili ya kuwachuja wale ambao hawajajitoa kweli ili kufanikiwa, wale ambao wanafanya kwa kujaribu tu.
Lakini wale waliojitoa kweli, wale ambao wapo tayari kupambana ili kupata wanachotaka na kufika wanakotaka kufika, hawana cha kuwazuia.
Wakikutana na kikwazo kwenye njia, wanakigeuza kuwa njia.
Wakikutana na ugumu wanautumia kuwa imara zaidi,
Wakikutana na kukatishwa tamaa wanazidi kuamini wako njia sahihi,
Wakikutana na wasichoweza wanajifunza au kutafuta wanaokiweza na kushirikiana nao.

Hakujawahi kuwepo kizuizi chochote kilichofaulu kumzuia yule ambaye ameamua kweli kufanikiwa.
Najua na wewe ni mmoja wa watu hao, umeamua kweli, ndiyo maana uko hapa.
Sasa basi, nenda kafanye kweli, nenda kageuze kila kikwazo kuwa njia, nenda kageuze kila udhaifu wako kuwa uimara kwako.
Na kamwe usiwe mtu wa kutoa sababu, visingizio au kuwalaumu wengine.
Wewe fanya kile unachopaswa kufanya, mpaka pale utakapopata unachotaka kupata.
Kataa kuzuiwa na chochote na utaona jinsi asili itakavyofungua milango mingi inayoonekana kujifunga mbele yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu nafasi ya uchoshi (boredom) kwenye ubunifu, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/02/2010

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,