“Pay bad people with your goodness; fight their hatred with your kindness. Even if you do not achieve victory over other people, you will conquer yourself.” — HENRI AMIEL
Unapolipa ubaya kwa wema,
Unapolipa chuki kwa upendo,
Lengo siyo kuwashinda wale wanaokufanyia hayo,
Bali lengo ni kujishinda wewe mwenyewe.
Mpumbavu yeyote anaweza kulipa ubaya kwa ubaya na chuki kwa chuki,
Na wapumbavu huwa wanafanya hivyo.
Inahitaji nguvu ya ziada kujizuia usilipe ubaya kwa ubaya na chuki kwa chuki.
Hivyo kila wakati kazana kujijengea udhibiti huo, siyo kwa sababu ya wale wanaokutendea, bali kwa sababu yako binafsi.
Unapomjibu mtu kwa ubaya na chuki,
Unakuwa umempa ushindi mkubwa,
Kwa sababu alikufanyia ubaya na chuki ili kuviibua ndani yako,
Unapomjibu hivyo, anakuwa ameshinda, lengo lake limefanikiwa.
Unapomjibu kwa wema na upendo, unakuwa umejishinda wewe mwenyewe.
Na yeye pia huenda ukamshinda, lakini hilo siyo lengo lako, hivyo isikusumbue.
Kazana kufanya kilicho sahihi mara zote, hata kama siyo rahisi kufanya.
Unapoweza kufanya, unakuwa umejishinda wewe mwenyewe.
Na ushindi wa kweli kwenye maisha, ni kujishinda mwenyewe.
Udhibiti wenye manufaa kwako, ni kujidhibiti mwenyewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu saa moja ya kufanya kazi, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/07/2015
Rafiki yako katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,