“Cling tooth and nail to the following rule: Not to give in to adversity, never to trust prosperity, and always to take full note of fortune’s habit of behaving just as she pleases, treating her as if she were actually going to do everything it is in her power to do.” – Seneca

Wakati sahihi wa kujiandaa na magumu ni pale mambo yanapokuwa mazuri.
Huo ndiyo wakati rahisi kwa wengi kujisahau na kuona mamno yataendelea kuwa mazuri.
Lakini ghafla mambo mazuri yanaisha na unaingia kwenye mambo magumu.

Dunia inazunguka,
Ndiyo maana kuna usiku na mchana, kiangazi na masika.
Kila kinachoenda juu huwa kinarudi chini.
Hizi ni kanuni za asili ambazo huwa zinafanya kazi mara zote.
Asili huwa inafanya yake, iwe unataka au hutaki.
Usiku na mchana utakuja kama asili ilivyojipanga na siyo kama wewe unavyotaka.
Kadhalika kwenye urahisi na ugumu, unakuja kama asili ilivyopanga.

Kwa kuwa asili haitakuambia lini mambo yatakuwa magumu au rahisi,
Ni muhimu wewe mwenyewe kuwa na maandalizi.
Wakati mambo yanakwenda vizuri, usijisahau, kuna wakati mambo yatakwenda vibaya.
Usisahau ulikotoka kwa kuona huwezi kurudi tena huko.
Kila wakati kuwa tayari kwa lolote linaloweza kutokea.
Maana hujui litakalotokea na wakati litakapotokea.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu ubinafsi, fungua kusoma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/13/2021

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,