“When you have done a good act and another has fared well by it, why seek a third reward besides these, as fools do, be it the reputation for having done a good act or getting something in return.” – Marcus Aurelius
Ipo kauli kwamba tenda wema na uende zako, usingoje shukrani.
Kauli hii ni sahihi sana, lakini haijaweka wazi kuhusu malipo ya wema.
Malipo ya wema siyo yule uliyemfanyia wema kukushukuru.
Bali malipo ya wema ni wewe kutenda wema huo.
Yaani ukishatenda huo wema, tayari ni malipo.
Kwa wewe kusukumwa kufanya kile ambacho unajua ni sahihi na kitamsaidia mwengine na kisha kukifanya, ni malipo tosha.
Kila unapotenda wema jua kwamba hutendi iwa ajili ya yule unayemtendea, bali unatenda kwa ajili yako binafsi.
Kwa sababu ndiyo kitu sahihi kwako kufanya, kwa sababu usipofanya baadaye itajutia.
Iwe mtu ametambua wema wako,
Iwe amekushukuru kwa ulichofanya,
Hayo hayakuhusu.
Kinachokuhusu ni kutenda wema, kwa sababu ni muhimu kwako.
Na katika kutenda wema wako, usiangalie unapata nini, bali angalia unatoa nini.
Kumbuka kila unachofanya ni kwa sababu yako kwanza kabla mwingine yeyote hajanufaika.
Hivyo jipunguzie msongo kwa kuacha kuwabeba wale ambao umewafanyia wema halafu hawakukushukuru.
Kila unapokunywa maziwa huwa unaenda kumshukuru ng’ombe kwa wema wake?
Je ng’ombe anaacha kutoa maziwa kwa sababu hajapewa shukrani?
Majibu ni hapana.
Ng’ombe anatoa maziwa kwa sababu ni asili yake,
Na wewe tenda wema kwa sababu ni asili yako.
Hiyo tu inatosha, usiangalie ya ziada.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu manadiliko siyo rahisi, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/16/2024
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,