“If you’re not enough before the gold medal, you won’t be enough with it.”
I remembered that if I wasn’t enough before being asked to participate in this prestigious event, then participating wasn’t going to make me enough. Being enough was going to have to be an inside job. – Anne Lamott
Mwandishi Anne Lamott kwenye kitabu chake cha Bird by bird anatuambia kwamba waandishi wengi hufikiri kwamba kazi zao zikishachapishwa basi watakuwa na furaha ya kudumu na kujiona wamekamilika.
Hivyo ndivyo na yeye alikuwa akifikiri kabla kazi zake hazijachapishwa,
Lakini baada ya kitabu chake cha kwanza kuchapwa, aligundua furaha ni ya muda mfupi, baada ya hapo maisha yanarudi vile vile.
Hivi ndivyo wengi tumekuwa tunajidanganya kwenye mafanikio,
Tunajiambia tukishapata tunachotaka basi tutakuwa na furaha ya kudumu na maisha yetu yatakuwa yamekamilika.
Huhitaji kwenda mbali kujua huo ni uongo.
Jiangalie wewe mwenyewe, angalia kitu chochote ulichokuwa unakisubiria kwa shauku kubwa, kwamba kitu hicho kikishatokea au ukishakipata basi maisha yako yatakuwa yamekamilika.
Labda ilikuwa kumaliza shule, au kupata kazi, au kupanda cheo, au kuoa/kuolewa au kununua gari au kuwa na nyumba au kuanza biashara au kustaafu.
Kabla ya vitu hivyo ulikuwa na matumaini makubwa sana, ukiamini ukishavipata basi maisha yako yatakuwa yamekamilika.
Ukapambana kweli na ukavipata au kuvifikia.
Na nini kikatokea baada ya hapo?
Ulifurahia kwa siku chache za mwanzoni na baada ya hapo maisha yakarudi kama awali.
Hakuna kitu chochote unachohangaika nacho sasa hivi ambacho ukikipata kitakukamilisha.
Hata kama unapambana kuwa bilionea, ukiyapata hayo mabilioni hayatakukamilisha.
Hivyo anza na ukamilifu ndani yako,
Anza na furaha,
Anza na utulivu na kujiamini,
Anza na uhuru.
Chochote ambacho huna sasa, jua hata ukipata unachotafuta hutakipata.
Huna uhuru sasa na unajiambia ukishakuwa bilionea utakuwa huru?
Endelea kujidanganya, lakini jua ule uhuru unaokosa sasa, utakuwa mara bilioni ukishayapata mabilioni.
Kadhalika furaha, kama huna furaha kabla hujafanikiwa, unapofanikiwa hali ya kutokuwa na furaha inakuwa kubwa zaidi.
Anza sasa kuyaweka maisha yako vile unavyotaka yawe, usisubiri chochote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuchagua eneo la kuhudumu, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/24/2032
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,