“I was repaid with evil for the goodness which I have done.” But if you love those for whom you did good, then you have already received your reward. Therefore, all that you do with love, you do for yourself. – Leo Tolstoy
Umewahi kumfanyia mtu wema na yeye akakulipa kwa ubaya?
Au ukamfanyia mtu wema na hakujali hata kukushukuru kwa wema uliofanya?
Umejisukuma kweli na kujiweka kwenye hatari ili wengine wanufaike, lakini baada ya kunufaika wanakuona wewe hufai?
Hizi ni hali ambazo zinaumiza sana.
Lakini zinaumiza pale unapokuwa hujajua kusudi la wewe kutenda wema.
Tuanze kwa kuangalia asili,
Umekuwa unakunywa maziwa, je umeshawahi kufuata ng’ombe na kuishukuru kwa maziwa inayotoa?
Unakula vyakula mbalimbali, je umewahi kutafuta mimea iliyozalisha vyakula hivyo na kuishukuru?
Majibu ni hapana,
Swali jingine, je ng’ombe wamewahi kugoma kutoa maziwa kwa sababu binadamu wanaoyatumia hawajawashukuru?
Jibu ni hapana, ng’ombe wanaendelea kutoa maziwa kila siku kwa sababu ni asili yao.
Tena wakiwa na maziwa na wasipoyatoa, yanawaumiza wao wenyewe ndani yako.
Hivyo pia ndivyo unavyopaswa kuwa kwenye wema,
Unapaswa kutenda wema siyo kwa sababu wengine wanaona au kukusifia,
Siyo kwa sababu wengine watajali na kukushukuru,
Bali kwa sababu ni kitu kilicho ndani yako, ni asili yako.
Unatenda wema kwa sababu hutaweza kwenda kulala kwa utulivu kwa kujua kuna mtu alikuwa kwenye hali ambayo ungeweza kusaidia lakini hukufanya hivyo.
Kutenda wema ni jambo la ubinafsi, kuepuka kusutwa na nafsi yako pale unapoacha kufanya kila unachojua kipo ndani ya uwezo wako.
Hivyo kuanzia sasa, acha kabisa kuumia pale unapotenda wema na wengine wasijali au kukulipa kwa ubaya.
Tenda wema bila mategemeo yoyote yale,
Tenda wema kwa kuangalia ndani yako na siyo kwa wengine.
Kwa njia hiyo, utakuwa na maisha tulivu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu mashujaa wapya ambao wamekuwa miungu wa zama hizi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/25/2033
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,