“And once you realize that you can do something, it would be difficult to live with yourself if you didn’t do it.” – James Baldwin
Ipo hadithi moja ya mtoto wa simba alipotea porini siku alipozaliwa,
Akaokotwa na kundi la kondoo na kukuzwa na kondoo hao.
Akawa anaishi kama kondoo, kila kitu anafanya kama kondoo.
Hata baada ya kuwa mkubwa na kuonekana wa tofauti na kondoo wengine,
Aliendelea kuishi kama kondoo.
Siku moja simba akiwa mawindoni akamuona simba huyo katikati ya kondoo.
Kondoo wengine walikimbia, lakini yeye alibali.
Ndipo simba alipomkaribia na kugundua ana tabia za kondoo.
Alimfundisha jinsi ya kunguruma kama simba,
Alipojaribu na kuweza, aligundua ana uwezo mkubwa kuliko alivyokuwa anaishi.
Na tangu hapo hakurudi tena kuishi na kondoo.
Maisha yetu ndiyo yalivyo,
Tulizaliwa tukiwa na uwezo mkubwa na wa tofauti, tukiwa na upekee.
Ila tukaangukia kwenye jamii ambayo imetugeuza kuwa kondoo.
Tunaendesha maisha yetu kama kila mtu kwenye jamii anavyoyaendesha.
Tunajiambia vitu ambavyo hatuwezi hata kabla hatujavijaribu.
Umefika wakati sasa wa kukataa kuwa kondoo,
Na siyo tu kukataa kwa utukutu,
Bali kwa kujua kile kilicho ndani yako,
Kujua uwezo wako mkubwa na wa kipekee,
Kujua nini unaweza kufanya ambacho wengine hawawezi,
Kisha kuendesha maisha yako kwa namna hiyo.
Kwa sababu ukishajua kweli kile unachoweza,
Ukishajua uwezo mkubwa ulio ndani yako,
Hutaweza kuyaishi tena maisha ya chini.
Ukishajijua ni simba, hutaweza kuishi tena baina ya kondoo.
Jamii haitaki ujue hilo,
Ndiyo maana kila wakati inahakikisha uko bize na mambo yasiyo na maana kwako,
Kukimbizana na mambo ya hovyo ili uchoke na usiangalie ndani yako kujua asili yako.
Kataa hilo sasa kwa kutambua asili yako na kuiishi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kila maamuzi ni mapya, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/26/2034