“Almost always, when we look deep into our souls, we can find there the same sins which we blame in others. If we do not find a particular sin in our soul, then we should look more closely, and we will find even worse sins there.” – Leo Tolstoy
Hakuna binadamu aliyekamilika,
Kila mmoja wetu ana madhaifu na mapungufu yake,
Ni madhaifu na mapungufu hayo ndiyo yanayopelekea mtu kufanya dhambi na makosa mbalimbali.
Hivyo siyo kwamba kuna wakosaji na watakatifu,
Wote ni wakosaji, ila wachache ndiyo makosa yao yanaonekana zaidi.
Hivyo kabla hujahukumu wengine kwa makosa yao, hebu jiangalie kwanza wewe mwenyewe.
Jichunguze kwa umakini na utagundua kuna makosa kama hayo au makubwa zaidi ambayo umekuwa unafanya.
Unataka kumhukumu mtu kwamba ana chuki au wivu,
Hebu angalia ndani yako, ni mara ngapi umeona wengine wanapiga hatua na badala ya kuwafurahia ukawa na chuki fulani, japo hukuionesha?
Tofauti yako na wengine ni kwamba umeweza kuficha chuki yako, wao hawajaweza.
Kwa kujua hili inatufanya tuwe wanyenyekevu na pia tuwe tayari kushirikiana na wengine katika kuwa bora zaidi.
Lakini hivyo sivyo maisha ya sasa yanavyoenda, hasa kwa zama hizi za mtandao.
Kila mtu ni hakimu kwenye maisha ya wengine,
Kila mtu yuko tayari kuhukumu na kulaumu wengine, hata kabla hajajua undani wa jambo.
Lakini pia haimaanishi kama tuna madhaifu basi tuyaendekeze,
Wala haituzuii kuwakemea wengine kwenye makosa yao kwa sababu na sisi tuna madhaifu.
Hii inatufundisha unyenyekevu na kutuwajibisha sisi wenyewe kabla hatujawaadhibu wengine.
Na muhimu zaidi, usitafute mtu aliyekamilika, hayupo, bali tafuta anayejua madhaifu yake na anakazana kuyafanyia kazi ili yasiwe kikwazo kwake.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuhangaika na mambo makubwa, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/27/2035
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,