“Many statements which are accepted as truth because they have been passed down to us by tradition look like truth only because we have never tested them, never thought about them in a more precise way.” – Leo Tolstoy
Mambo mengi ambayo tunaamini ni kweli, ni kwa sababu ndivyo tulivyopokea.
Tunaamini ni kweli kwa sababu tumeambiwa hivyo.
Huwa hatuhangaiki kuhoji na kudadisi kama kile tunachoambiwa ni kweli kina ukweli.
Kwa kupokea ukweli tunaopewa bila kuuhoji na kudadisi, ndiyo kikwazo kikubwa kwenye uhuru na mafanikio.
Wale wote walioleta mabadiliko duniani na hata kufikia mafanikio makubwa, walihoji na kudadisi ukweli uliokuwa unaaminiwa na kila mtu.
Mwanzo walionekana kama wana ugonjwa wa akili, wakapingwa, kufungwa na kuuawa.
Lakini baadaye ukweli ulikuja kujiweka wazi.
Kuna kipindi watu waliamini dunia siyo duara,
Kuna kipindi watu waliamini jua linaizunguka dunia,
Kuna kipindi watu waliamini kusafiri kwa gari au treni iendayo kasi mtu atakufa.
Kuna kipindi watu waliamini binadamu hawezi kupaa angani.
Lakini sasa ushahidi uko wazi, yote hayo hayakuwa sahihi.
Usikubali kirahisi kila ukweli unaopewa,
Badala yake hoji na dadisi ili kujua kama ni kweli, kweli.
Sayansi na teknolojia zinapiga hatua zaidi kwa sababu ya watu kuwa tayari kuhoji, kudadisi na kutafiti bila ya mipaka.
Hilo pia ndiyo unalohitaji kwenye maisha yako,
Usiwe kama wengine kwa kupokea ukweli wa kupewa na kuridhika nao, badala yake hoji, dadisi, tafiti.
Hata yale ambayo unaamini juu yako,
Labda unaamini huwezi kufanya kitu fulani, usikubali tu kirahisi, jaribu kufanya uone.
Uzuri ni kwamba ukweli uko wazi kwa kila mtu,
Ila wachache ndiyo wanaoutafuta,
Na hao ndiyo wanaofanikiwa sana.
Kuwa mmoja wa hao wachache.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu madhara ya mafanikio ya haraka, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/05/2044
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani.