“You could choose no worse way to guide your life than to follow the opinions of other people.” – Leo Tolstoy
Hakuna njia mbovu ya kuendesha maisha yako kama kufuata maoni ya watu wengine.
Utakuwa umechagua maisha ya hivyo na yasiyo na msimamo.
Kwa sababu hata uchague kufanya nini, kuna watu watakuwa na maoni ya kupinga unachofanya.
Kumbuka hadithi ya mke na mume waliokuwa wanasafiri na punda.
Waliamua kupanda punda huyo, wakakutana na watu wakawaambia wana roho mbaya, watu wawili wanapandaje punda moja.
Wakaona isiwe shida, wakashuka na kutembea kwa miguu, wakakutana na watu wakawaambia ni wajinga, hawajui matumizi ya punda.
Mwanaume akaamua mke wake apande punda na yeye atembee kwa miguu, watu wakamwambia ni mume bwege, anatembeaje kwa miguu huku mke wake amepanda punda.
Mwanaume akaamua apande punda na mke atembee kwa miguu, watu wakasema ni unyanyasaji wa kijinsia.
Wakaona isiwe tabu, bora wambebe huyo punda, watu wakawaambia wamevurugwa, wanambebaje punda badala ya wao kubebwa na punda?
Hivyo ndivyo maisha yalivyo,
Kwa kila unachochagua kufanya, watu watakuwa na maoni yao.
Sasa kama utafanya kwa kufuata maoni ya wengine, utaumia na hutaweza kupata unachotaka.
Unachopaswa kujua ni kwamba wale wanaokupa maoni, hawajui nini hasa unachotaka.
Hivyo endesha maisha yako kwa mipango yako,
Fanya kile kilicho sahihi na usitake kumridhisha kila mtu.
Fanya yako na waache watu wawe na maoni yao.
Maana maoni ya watu huwa hayana mwisho.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kujiwekea vigezo vya kufanya maamuzi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/06/2045
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani.