“A most dangerous temptation is the temptation to pre pare to live, instead of living. The future does not belong to you. Therefore, remember to live the best way you know now. The only perfection necessary is perfection in love, which can be reached only in the present. It’s why we came into this world.” – Leo Tolstoy
Watu wengi wamepoteza maisha yao kwa kujiandaa kuishi na maisha yao kufika ukingoni kabla hata hawajaanza kuyaishi.
Usikubali hili litokee kwako,
Usiyapoteze maisha yako,
Yaishi maisha yako sasa, kwenye wakati uliopo.
Fanya kila unachopaswa kufanya sasa,
Na usiahirishe chochote kwa ajili ya kesho.
Kwa sababu hakuna kesho,
Kwa kuwa jana ulisema utafanya kesho, na ukaiona leo, siyo uhakika kwamba utaiona tena kesho nyingine.
Hivyo itumie leo na sasa vizuri.
Ishi kwa namna bora unayoweza kuishi sasa, kwa pale ulipo sasa.
Kila unachokifanya, kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana.
Usiache chochote kizuri kwa ajili ya kesho au siku zijazo,
Wakati wako ni sasa.
Usisubiri uwe mkamilifu ndiyo uyaishi maisha yako sasa.
Ukamilifu pekee unaohitaji ni wa upendo.
Ulishakuwa na upendo wa kweli, unaotoka ndani yako kweli, mengine yote yatakwenda vizuri.
Hata kama mambo ni magumu kiasi gani,
Hata kama unapitia changamoto kubwa kiasi gani,
Kama una upendo mkuu ndani yako, kwa kujipenda mwenyewe, kupenda wengine na kupenda kile unachofanya, basi maisha yako yatakuwa bora sana.
Huwezi kutunza upendo kwa ajili ya baadaye, upendo unauonesha kwenye wakati ulionao sasa
Ishi sasa, ndiyo nafasi pekee uliyonayo kwenye maisha yako, itumie vyema.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuweka kazi kwenye mahusiano, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/09/2048
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.