“You should not be upset by the sight of wisdom being criticized. Wisdom would not be real wisdom if it did not reveal the stupidity of a bad life, and people would not be people if they endured this revelation without criticism.” – Leo Tolstoy

“Dogs bark at what they cannot understand.” – Heraclitus

Ni kawaida kwa watu kuipinga na kuikataa hekima.
Wanafanya hivyo kwa sababu hawaielewi,
Na pia kwa sababu hekima inaonesha upumbavu wao.
Kwa kuwa hekima inasimama kwenye ukweli,
Na kwa kuwa ukweli unaumiza,
Basi hekima huwa inashambuliwa na kukosolewa.
Hilo halipaswi kukufanya wewe uiache hekima.

Kama ambavyo mbwa hubweka pale wanapokutana na wasichokielewa,
Ndivyo watu hushambulia hekima na ukweli.
Watu huiona hekima kama hatari kwao, kwa sababu inaweka wazi upumbavu wao.

Watu huwa wanajidanganya mpaka wanaishia kuamini uongo wao.
Na hapo maisha yao yanakwenda murua kwa uongo walioukubali.
Hekima inapokuja na kuanika uongo wao, inawafanya waone maisha yao yote yamejengwa kwenye msingi wa uongo.
Hawawezi kukubaliana na hilo kitahisi, hivyo watapambana na hekima na kuonesha maisha yao yako sahihi.

Asubuhi ya leo, tafakari hili na kisha chukua hatua zifuatazo;
👉🏽Kuwa tayari kuipokea hekima, hata kama inapingana na kile ambacho umekuwa unakiamini kwa muda mrefu.
👉🏽Usiiache hekima kwa sababu wengine wanaishambulia na kuipinga. Haiwezi kuwa hekima kama haianiki upumbavu wa watu. Na watu hawapo tayari kuona upumbavu wao ukianikwa.
👉🏽Unapokuwa upande wa hekima, usibishane na wale wanaoipinga, waeleze ukweli ni upi na kama wataukataa ni juu yao. Uzuri wa ukweli ni huwa haupotei, unaweza kuchukua muda, lakini siku moja utaonekana wazi kabisa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni jinsi ya kuwa mtu asiyevurugwa, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/12/2051

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.