“When jarred, unavoidably, by circumstance revert at once to yourself and don’t lose the rhythm more than you can help. You’ll have a better grasp of harmony if you keep going back to it.” —MARCUS AURELIUS
Chagua aina ya maisha unayotaka kuyaishi na utaratibu wa kuyaishi maisha hayo, kisha ishi utaratibu huo kila siku.
Lakini tambua kwamba siku hazilingani, kuna siku mambo yaliyo nje ya uwezo wako yatakuvuruga.
Cha msingi ni kuhakikisha unarudi kwenye utaratibu wako.
Unapotelezs usipotee kabisa, badala yake jisukume kurudi kwenye utaratibu wako wa kila siku.
Kuteleza siyo kubaya na hata kuanguka siyo mwisho.
Bali unapobaki pale unapoanguka ndiyo unakuwa umeuchagua mwisho wako.
Wajibu wako mkuu ni kuijua njia sahihi kwako na kurudi kwenye njia hiyo kila unapojikuta umepotea.
Wengi wanapotea kabisa kwa sababu hawajachagua njia kuu kwao, hawajui wapi wanapokwenda, hivyo chochote kinachokuja mbele yao kinakuwa ni sawa.
Usiruhusu kwako iwe hivyo,
Ndiyo maana ni muhimu kila siku kufanya tathmini ya siku yako,
Kupitia kila ulichofanya kwenye siku hiyo,
Na kuangalia kinakufikishaje kwenye mpango wako mkuu
Kama utagundua kwenye siku yako umefanya yasiyokufikisha unakokwenda, siku inayofuata usifanye tena kitu hicho.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu namna sahihi ya kuyaona mambo, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/19/2058
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.