“You should never be ashamed of any work, even the low est and dirtiest, but you should be ashamed only of the dirtiest moral state, that is which is the necessary result of labor of others.” Leo Tolstoy
Kamwe usiionee aibu kazi ya aina yoyote ile.
Hata kama ni kazi inayoonekana ni ya chini kabisa,
Kama unapaswa kuifanya basi ifanye kwa upendo na moyo mmoja,
Ifanye kwa kujituma na juhudi kubwa.
Kwa njia hiyo utaweza kuzalisha matokeo bora kwako na kwa wengine pia.
Kazi ndiye rafiki wa kweli,
Huwapenda wanaoipenda,
Na kuwakimbia wanaoikimbia.
Hakuna kazi nzuri au mbaya, bali mtazamo wa mfanyaji wa kazi ndiyo unampelekea aone ni nzuri au mbaya.
Hakuna kazi ya heshima na isiyo ya jeshima, bali vile mfanyaji anavyoichukulia ndivyo wengine pia wanaichukulia.
Kazi yoyote usiyoiheshimu, na wengine pia hawataiheshimu.
Chagua kazi unayotaka kuifanya, kisha ifanye kwa juhudi, weka upendo na iheshimu.
Wengine nao watalazimika kuiheshimu kama unavyofanya wewe.
Usiwaendekeze wale wanaodharau kazi yako, watapata funzo na kuiheshimu.
Kitu pekee umachopaswa kukionea aibu na kukikataa ni kutokuwa na kitu cha kufanya.
Hapo ndipo unapopata muda wa kufikiria na kutenda yasiyo sahihi
Ukiyatafakari maisha yako, utagundua kila baya au uovu umewahi kufanya, ni kwa sababu hukuwa umetingwa na kazi ya kufanya.
Kuliko usiwe na cha kufanya kabisa, fanya chochote.
Kama usemi ulivyo, mtembea bure siyo sawa na mkaa bure.
Kama kuna bahati, itakuwa rahisi kwa mtembea bure kuliko mkaa bure.
Ipende na kuiheshimu kila aina ya kazi, ifanye kwa kujituma na itakuwa na mchango bora kwako na kwa wengine pia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu mtego uliopo kwenye furaha, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/24/2063
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.