“It is as easy to deceive oneself without perceiving it as it is difficult to deceive others without their perceiving it.” — François duc de La Rochefoucauld
Ni rahisi sana kwako kujidanganya mwenyewe bila ya kujua kwamba unajidanganya.
Ni vigumu sana kuwadanganya wengine, bila ya wao kujua kwamba unawadanganya.
Hivyo kwa kila namna unajidanganya.
Unajidanganya mwenyewe bila kujua,
Huku pia ukiwadanganya wengine na kuamini hawajui,
Kumbe wanajua na wanakuchora tu.
Njia sahihi ya kuyaishi maisha yako ni kusimama kwenye ukweli,
Kuujua ukweli na kuuishi.
Kufanya kile kilicho sahihi.
Anza kwa kuwa mkweli kwako na itakuwa rahisi kuwa mkweli kwa wengine.
Tambua hakuna mtu mwingine unayeweza kumdanganya isipokuwa wewe mwenyewe.
Hivyo uongo hauna manufaa yoyote kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu mstari mwembamba uliopo kati ya kilicho sahihi na kisicho sahihi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/27/2066
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.