“The task of a philosopher: We should bring our will into harmony with whatever happens, so that nothing happens against our will and nothing that we wish for fails to happen.” —Epictetus
Kinachofanya ukwame na kuvurugwa kwenye maisha, ni matokeo unayoyapata kuwa tofauti na matakwa yako.
Kila unapofanya kitu, huwa unategemea kupata matokeo fulani.
Inapotokea matokeo yanayokuja ni tofauti na matakwa yako, basi unakwazika, unavurugwa na kuona dunia haiko sawa.
Kama unataka kuwa na utulivu na usivurugwe na chochote, basi hakikisha chochote hakitokei kinyume na matakwa yako.
Na hufanyi hivyo kwa lilazimisha umachotaka kitokee,
Bali unafanya hivyo kwa kukubali kila kinachotokea.
Yaani matokeo yoyote unayoyapata, basi yapokee kama ndiyo uliyokuwa unategemea kupata.
Weka juhudi unazopaswa kuweka na jisukume kweli kwenye juhudi.
Lakini matokeo yanapokuja, yapokee kwa shauku kubwa, kwamba ndiyo matokeo uliyotaka.
Hata kama siyo matokeo uliyotegemea, wewe yapokee kama ndiyo uliyategemea.
Baada ya kuyapokea, jiulize hatua zipi zaidi unapaswa kuchukua kisha zichukue.
Haukubaliani na kila matokeo ili uwe mzembe,
Bali unakubaliana nayo ili uwe na utulivu na uweze kuchukua hatua sahihi.
Kama tunavyojifunza kila mara, asili haifuati matakwa yetu.
Hivyo kukasirika na kuvurugwa kwa sababu umeweka juhudi lakini matokeo hujayapata ni kupoteza muda wako.
Kila kinachotokea ndiyo ulichokitegemea, kisha kifanyie tathmini na kupanga hatua zaidi za kuchukua. Hiyo ndiyo namna ya kuwa na maisha tulivu wakati wote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kitendawili cha maamuzi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/28/2067
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.