“Consort with the crowd is harmful; there is no person who does not make some vice attractive to us, or stamp it upon us, or taint us unconsciously therewith. Certainly, the greater the mob with which we mingle, the greater the danger.” – Seneca

Wewe pekee ndiye unayejua nini unataka kwenye maisha yako
Wewe pekee ndiye unayejua misimamo na maadili unayotaka kujijengea.
Wewe pekee ndiye unayejua kipi sahihi na siyo sahihi kwako.
Unapofuata mkumbo na kufanya yale wengine wanafanya, unapoteza upekee wako na kuwa kama wengine.

Hilo ni hatari kwa sababu kundi kubwa la watu huwa halifikiri,
Huwa linaenda kwa mkumbo na mwisho wote huangamia.

Pambana kusimama wewe kama wewe,
Hata kama kila mtu anapingana na wewe,
Unajua unachotaka na unajua kilocho sahihi kufanya, fanya hayo.

Kazana kuyaishi maisha yako, hayo yatakupa ridhiko kubwa kuliko kukazana kuenea kwenye kundi kubwa la watu.
Usiogope wengine watakuchukuliaje, ogopa kutokuyaishi maisha yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuweka kazi, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/31/2070

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.