“Soldiers who stand idle in a shelter during a battle as re inforcements will try to involve themselves in almost any activity in order to distract themselves from the impending danger. It seems to me that people who want to save them selves from life behave like these soldiers: some distract themselves with vanity, some with cards, politics, laws, women, gambling, horses, hunting, wine, or state affairs.” – Leo Tolstoy

Kitu chochote unachofanya, ambacho hakina mchango kwenye kufikia mafanikio makubwa unayotaka kufikia kwenye maisha yako, ni kuyatoroka maisha.

Matumizi ya vilevi, kufuatilia habari, kuzurura kwenye mitandao ya kijamii, mabishano na kufuatilia maisha ya wengine, yote hayo ni kuyatoroka maisha yako.

Swali muhimu la kujiuliza kila wakati ni kwa nini unayatoroka maisha yako?
Mara nyingi unajikuta umeshayatoroka maisha bila ya wewe mwenyewe kujua,
Unajikuta umeshazama kwenye usumbufu na umeacha kufanya yale muhimu.

Ni wakati sasa wa kujikamata pale unapoyatoroka maisha na kujilazimisha kurudi kufanya yaliyo muhimu.
Kila unapoianza siku yako, orodhesha yale unayokwenda kufanya kwenye siku hiyo na yapangie muda utakayoyafanya.
Huo ndiyo unakuwa mwongozo wako wa siku na mara kwa mara jikague kama bado uko kwenye mwongozo wako au umeshatoroka.

Haimaanishi kwamba unapaswa kufanya yale muhimu masaa 24 kwa siku,
Usiseme hapa kwamba hutoroki bali unapumzika.
Maana hakuna mapumziko unayoyapata kwa kutumia vilevi, unakuwa mchovu zaidi baada ya vilevi hivyo.
Kadhalika hakuna mapumziko unayoyapata kwa kuzurura mitandaoni, kufuatilia habari, kuangalia tv na mengine kama hayo. Unajikuta umevurugwa zaidi baada ya hayo kuliko kuwa kwenye utulivu.

Kwenye kila siku yako tenga muda wa kupumzika na pumzika kweli, siyo kufanya mambo yanayokuchosha au kukuvuruga zaidi.
Mapumziko yanapaswa kukupa utulivu wa akili na nguvu ya mwili.

Usikubali kuendelea kujirudisha nyuma kwa kuyatoroka maisha yako,
Weka vipaumbele vyako kwa usahihi na visimamie hivyo. Usitoke nje ya vipaumbele vyako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu gharama ambatanishi, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/01/207

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.