“The closer people are to the truth, the more tolerant they are of the mistakes of others.” – Leo Tolstoy

Kadiri unavyoukaribia ukweli, ndivyo unavyokuwa mvumilivu kwenye makosa ya wengine.
Unazidi kuwa mkali kwako mwenyewe, huku ukiwavumilia wengine kwa makosa wanayofanya.

Ukweli unakupa nafasi ya kujua jinsi wengi walivyo gizani,
Utaona kwamba wengi wanakosea siyo kwa makusudi, bali kwa kutokujua vyema zaidi.

Ukweli unakifanya uone uhalisia kama ulivyo na siyo kama unavyotaka kuuona wewe.

Wasiojua ukweli huwa na matarajio yasiyowezekana.
Hutaka kila mtu awe kama wao, aamini wanachoamini na kufanya kama wanavyotaka.
Kwa kuwa hilo haliwezi kutokea, basi watu hao wasiojua ukweli hujikuta wakikwazika mara zote.

Wanaojua ukweli wanakuwa huru, kwa kuwaweka wengine huru pia.
Wanakubali wengine waamini wanachotaka kuamini na kufanya wanachoona ni sahihi kwao.
Japokuwa wanaujua ukweli, hawaulazimishi kwa wengine.

Asubuhi hii tafakari jinsi ambavyo umekuwa unawachukulia wengine, hasa makosa yao na kwenye maeneo mnayotofautiana,
Kisha jiulize kama upo kwenye ukweli au siyo.
Jibu utakalopata, likusukume kuchukua hatua sahihi, ya kuwa kwenye ukweli.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kutokujilinganisha na kiwanda au taasisi, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/02/2072

Rafiki yako,
Kocha Dr. Makirita Amani.