“The future does not really exist. It is created by us in the present.” – Leo Tolstoy
Adui mkubwa wa mafanikio ya wengi ni kesho.
Kuacha kufanya yale mtu amepanga kwa kujiambia atafanya kesho imekuwa inawahadaa wengi.
Cha kusikitisha ni kwamba, hiyo kesho huwa haifiki.
Hivyo ahadi ya nitafanya kesho huwa ni endelevu.
Unachopaswa kujua ni kwamba hakuna kesho.
Kesho iko ndani yako leo.
Hivyo kama utashindwa kufanya kitu leo, usijidanganye kuweza kukifanya kesho.
Maana wewe wa leo ndiyo wewe wa kesho,
Kushindwa kufanya leo na kujiambia utafanya kesho ni kujidanganya tu.
Kesho tayari unayo leo,
Unapopanga kufanya kitu, kifanye kama ulivyopanga na siyo kukipeleka kesho.
Kesho tayari iko ndani yako leo na usitegemee miujiza yoyote kwenye hiyo kesho.
Hata kama hutaweza kufanya na kukamilisha, wewe anza kufanya leo.
Ukishaanzisha mwendo ni rahisi kuendelea kuliko kutokuanza kabisa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu magugu yasiyoisha, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/06/2076
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.