“Be more careful not to Miss once than to Hit a hundred times” – François Duc de La Rochefoucauld
Kwenye safari yetu ya mafanikio,
Huwa tunaweka mkazo kwenye kufanya.
Kwa kuwa mafanikio ni zao la msimamo na matokeo ya hatua ndogo ndogo zinazorudiwa kwa muda mrefu, msimamo kwenye ufanyaji ni kitu muhimu.
Kwetu sisi binadamu, kile tunachorudia kufanya mara nyingi hugeuka na kuwa tabia.
Hivyo baadaye huwa siyo vigumu tena kufanya kama awali.
Hiyo inapelekea kufanya isiwe vigumu.
Japo kufanya ni eneo muhimu kwenye mafanikio,
Kuna eneo jingine muhimu pia lakini tumekuwa hatulipi uzito unaostahili
Eneo hilo ni kuepuka kuacha kufanya.
Katika eneo hili, unapaswa kuhakikisha huachi kufanya hata mara moja.
Kwa sababu ukishaacha mara moja, basi jua utaacha tena na tena na tena, na baadaye inakuwa tabia.
Kama ilivyo kwenye kufanya, ni ngumu mara ya kwanza, lakini baada ya hapo inakuwa rahisi.
Kadhalika kwenye kuacha kufanya, kama hujawahi kuacha kufanya, itakuwa vigumu kwako kuacha kwa mara ya kwanza,
Lakini ukishaacha mara moja, wakati mwingine huwa siyo ngumu kuacha
Hivyo jukumu lako kuu, kazi yako kubwa ni kuhakikisha huachi kufanya.
Kama umejiwekea utaratibu wa akiba kila kipindi fulani, fanya kama ulivyopanga bila kuacha hata mara moja.
Kwenye kila siku yako, chagua kitu utakachokifanya bila kuacha hata siku moja,
Inaweza kuwa tahajudi, uandiashi, usomaji, mazoezi, kazi fulani n.k.
Kama hujawahi kuacha kufanya, ni vigumu sana kuacha, lakini kama umewahi kuacha kufanya hata mara moja tu, mara ya pili huwa ni rahisi.
Tengeneza mnyororo ambao hutauvunja,
Na siku unashawishika kuacha kufanya, uangalie mnyororo wako na jiulize kama kweli uko tayari kuvunja mnyororo huo ulioutengeneza kwa muda mrefu.
Fanya kila ulichopanga kama ulivyopanga na kuwa makini zaidi usishawishike kuacha hata mara moja.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu umaarufu na uaminifu, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/07/2077
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.