Maisha ni magumu, lakini huwa tunayafanya kuwa magumu zaidi kwa baadhi ya mambo tunayohangaika nayo.
Wastoa, hasa mwanafalsafa Epictetus alikuwa akisisitiza sana kujua mambo yaliyo ndani ya uwezo wako na kujishughulisha nayo na kujua yale yaliyo nje ya uwezo wako na yasikusumbue.
Katika mwendelezo wa hilo, Epictetus anatushirikisha kanuni ya kuwa na maisha rahisi, kanuni hiyo ni kama ifuatavyo;
Usiache kabisa na wala usifanye kupitiliza, kwa kila jambo, fanya kwa kiasi.
Waache wengine na machaguo yao, usijihangaishe nayo.
Yafanye machaguo yako kuwa siri yako, usitangaze na kuweka zazi kila jambo lako.
Usifikirie wewe ni bora au muhimu kuliko wengine, haijalishi una nafasi kubwa kiasi gani.
Ni mambo rahisi haya, na tunayoyajua, lakini swali ni je tunayaishi?
Viashiria kwamba huishi misingi hii ni kujikuta kuwa kwenye hali ya kutokuelewana na wengine, kwa sababu unawalazimisha wawe kama unavyotaka wewe.
Pia kukasirishwa na kile wanachofanya wengine, ni kiashiria kwamba hujakubali machaguo yao.
Jikague kwenye maisha yako, angalia changamoto nyingi unazokutana nazo na utagundua kuna jambo kati ya haya tuliyojifunza hapa unaenda kinyume nalo. Lirekebishe na utaweza kuwa na maisha tulivu.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Machaguo yangu ni siri yangu.
Shukrani sana kocha kwa makala hii.
LikeLike
Kuna faida kubwa katika kusoma na kujifunza,na Maneno ya mwanafalsafa Epictetus yanausadiki ukweli ambao siku zote utaendelea kusimama,”Yafanye machaguo yako kuwa siri yako,usitangaze na kuweka wazi kila jambo,ni Maneno muhimu sana ya kuyaishi na kujiletea mafanikio.asante sana kocha.
LikeLike
Hakika Beatus.
Tumekuwa tunatengeneza matatizo mengi kwa kupuuza misingi hiyo rahisi.
LikeLike