“I keep silence about many things, for I do not want to put people out of countenance; and I am well content if they are pleased with things that annoy me.” – Johann Wolfgang von Goethe
“Closed thoughts and an open face. Smile at everyone, and don’t tell them what you’re thinking.” – Sir Henry Wootton
Kwa sababu tupo kwenye zama za uwazi, haimaanishi uweke wazi kila unachofikiri.
Kwa sababu mitandao ya kijamii inakuuliza unafikiri nini na kukushawishi uwashirikishe wengine, haimaanishi ni sahihi kufanya hivyo.
Hupaswi kuweka wazi kila unachofikiri.
Hata kama una uhakika unachofikiri wewe ndiyo ukweli na wanachofikiri wengine siyo sahihi.
Ni watu wachache sana walio tayari kuupokea ukweli.
Wengi wanafurahia kuendelea kuamini kile ambacho wamekuwa wanaamini miaka mingi na hawataki kuyumbishwa kwenye imani hizo.
Hivyo kaa kimya kwenye yale ambayo unatofautiana na wengi.
Huhitaji kubishana na kila mtu kwa sababu wewe uko sahihi,
Kumbuka wewe siyo kiranja wa dunia,
Utaishia kutokuelewana na watu kwa jambo ambalo wao wenyewe hawatabadilika.
Kama anavyotuambia Goethe huhitaji kukosana na kila mtu kwa sababu mnafikiri au kuamini tofauti, kuwa tayari kukubali pale kile unachoona cha hivyo, wengine wanaona cha thamani.
Na kama anavyotushauri Wootton, tabasamu na kila mtu na siyo lazima umweleze kila mtu kile unachofikiri.
Chagua watu unaoweza kujadili nao mambo makubwa na magumu, siyo kila mtu ana uwezo huo.
Chagua watu ambao wanaweza kupokea ukosoaji au ushauri wako, siyo kila mtu anaweza hivyo.
Wengine unapaswa kukubaliana nao tu, huku ukitabasamu na kuendelea na yako.
Huwezi kuifanya dunia na kila mtu awe kama unavyotaka wewe, hata kama ni kwa manufaa yao.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu wewe wa leo na siyo wa jana wala kesho, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/13/2083
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.