“Those who apply themselves too closely to little things often become incapable of great things.” – François Duc De La Rochefoucauld
Kinachokuzuia wewe usifanye makubwa,
Ni kuhangaika na mambo madogo madogo.
Unatia bidii na umakini kwenye mambo madogo na yasiyo na tija, unayafanya vizuri kabisa, lakini hayana mchango wowote kwako.
Unaimaliza siku yako uliwa umechoka, lakini unapoangalia hakuna kikubwa ulichofanya.
Miaka inakatika na ukijitathmini huoni hatua unazopiga.
Mapenzi yako kwenye vitu vidogo vidogo yanakukwamisha mno.
Kila unapoianza siku yako, unakuwa na vitu vitatu vyenye ukomo, muda, nguvu na umakini.
Unaoanza siku ukiwa na masaa 24 mbele yako, na huwezi kuongeza hata dakika moja. Muda unaoutumia kufanya kitu A huwezi kuutumia tena kufanya kitu B kwa wakati huo huo. Hivyo kama unachofanya siyo muhimu, kile muhimu hakipati muda.
Unaianza siku ukiwa na nguvu za kutosha, kama betri ya simu iliyojaa chaji.
Kila unachofanya kwenye siku yako, kinapunguza nguvu zako. Hivyo unapohangaika na yasiyo muhimu, unachoka na kushindwa kufanya yaliyo muhimu.
Umakini wako unaweza kuupeleka kwenye kitu kimoja.
Akili yako haiwezi kufikiri vitu viwili kwa wakati mmoja.
Hivyo akili inapotawaliwa na mambo madogo madogo, makubwa yanakosa nafasi.
Mambo hayo madogo yanayokuwa kikwazo kwako ni yapo?
Kufuatilia habari, mitandao ya kijamii, udaku, majungu, mabishano na starehe mbalimbali.
Chochote unachokipa muda, nguvu na umakini wako, na hakichangii wewe kufika kwenye mafanikio makubwa, ndiyo kikwazo kwako.
Vitambue vikwazo vyako na usiendee kuvipa nafasi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kauli ya kishujaa na itakayokupa uhuru (kwa ukurasa huu naomba uweke coment yako yenye kauli ya kishujaa kwako) fungua hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/16/2086
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.