“We cannot prevent birds from flying over our heads, but we can keep them from making nests on top of our heads. Similarly, bad thoughts sometimes appear in our mind, but we can choose whether we allow them to live there, to create a nest for themselves, and to breed evil deeds.” — Martin Luther
Huwezi kuwazuia ndege wasiruke juu ya kichwa chako,
Ila unaweza kuwazuia wasijenge kiota juu ya kichwa chako.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye fikra mbaya na hasi,
Huwezi kuzizuia usiwe nazo kabisa, ila unaweza kuzizuia zisiweke kambi kwenye akili yako.
Kupata fikra mbaya na hasi mara moja moja ni hali ya kawaida kwetu binadamu.
Ni pale tunapoziruhusu zikae kwenye akili yetu muda wote ndiyo zinaharibu kabisa mtazamo wetu.
Kuwa na hali ya hofu hasa unapokabiliana na jambo jipya na kubwa ni hali ya kawaida,
Lakini unapozipa nafasi hofu hizo ndiyo zinakuwa kikwazo kwako kupiga hatua na kufanikiwa.
Hivyo usijisikie vibaya pale fikra mbaya zinapopita kwenye akili yako,
Fikra hasi, za kukata tamaa au za hofu,
Mbaya ni pale zinapoweka kambi na kubadili mtazamo wako.
Wajibu wako ni kuhakikisha fikra hizo zinapita na unarudi kwenye fikra zilizo sahihi.
Tafakari, tahajudi na kujifunza vitu chanya ni njia bora ya kuhakikisha fikra mbaya haziweki kambi kwenye akili yako.
Tumia njia hizo ili uendelee kubaki imara.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuzuia umri wako usiwe kikwazo, wakati wa ujana na wakati wa uzee, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/20/2090
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante Sana kocha, pamoja na changamoto mbali mbali tunazopitia hakika bado kuna nafasi nzuri ya kufanikiwa na kusonga mbele.
LikeLike