“A clever man ought to so regulate his interests that each will fall in due order. Our greediness so often troubles us, making us run after so many things at the same time, that while we too eagerly look after the least we miss the greatest.” – François Duc De La Rochefoucauld

Kitu kikubwa kinachokusumbua kwenye maisha yako ni tamaa.
Hizo zinakufanya uhangaike na mambo mengi kwa wakati mmoja,
Halafu mwisho wa siku hakuna kikubwa unachokamilisha.
Wakati unahangaika na mambo madogo madogo, mambo makubwa yanakupita.

Mara nyingi umekuwa unafanya kitu, siyo kwa sababu ndiyo kinachotoka ndani yako,
Ila kwa sababu umeona wengine wanafanya au wanacho na wewe ukaingiwa tamaa.
Na mara zote unapofanya mambo kwa tamaa, unaishia kushindwa au hata ukishinda, hufurahii ushindi huo, kwa sababu siyo kitu kilichotoka ndani yako.

Angalia wale wanaohangaika na kukimbizana na fursa mpya kila siku, huwa wanafika wapi?
Pamoja na mahangaiko mengi, mwisho wa siku wanajikuta pale walipoanzia.
Na wakati wanahangaika na fursa hizo, wanaacha kufanya kile ambacho ni muhimu kwao, kinachotoka ndani yao na hapo ndipo wanaishia kushindwa.

Unapaswa kudhibiti tamaa zako, kwa kuhakikisha husukumwi na mihemko, hufanyi maamuzi kwa kile unachoona kwa wengine, bali kile kinachoanzia ndani yako.

Ndani yako tayari unayo ya kutosha, ambayo ukiyafanyia kazi utapiga hatua sana, acha kupoteza muda kwa kuhangaika na ya nje

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kujiwekea ukomo kwenye matumizi ya muda wako, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/21/2091

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.