Fanya kazi kwa juhudi na maarifa na utafika kwenye mafanikio makubwa. Huu ni ushauri ambao kila mtu anayetaka mafanikio ya uhakika huwa anapewa.

Lakini wengi huwa hawauelewi ushauri huu na hivyo kuishia kuumia.

Ushauri unaeleza wazi kwamba fanya kazi kwa juhudi na maarifa, ukisisitiza upande wako wewe ni kuweka kazi.

Kuhusu matokeo unayopata, hapo ndipo wengi wanapopotea. Wengi wanataka wakifanya kazi matokeo wayaone hapo hapo na iwapo matokeo yatachelewa basi wanaona kazi waliyofanya siyo sahihi, wengi wanakata tamaa na kuacha.

Unachopaswa kuelewa ni kwamba hakuna kazi unayoweka ambayo inapotea, unaweza usione majibu sasa, lakini kuwa na uhakika kwamba majibu yatakuja. Yatakuja lini? Hiyo siyo kazi yako, wewe weka kazi, kisha amini majibu yatakuja na yasubiri yaje.

Usiilazimishe dunia iende kama unavyotaka wewe, huwezi, utajiumiza. Kulazimisha matokeo unayoyataka na kwa wakati unaotaka ni kujiandaa kuumia.

Wewe weka kazi, hicho ndiyo kilicho ndani ya uwezo wako, kisha kuwa na subira wakati dunia inafanya yake ili kukuletea wewe majibu sahihi.

Wakati mwingine kulazimisha kwako majibu, kunakuletea majibu yasiyo sahihi. Hivyo kuwa mpole na mvumilivu huku ukiendelea kuweka kazi na hakuna unachofanya kinachopotea.

Kuweza kuishi kwa msingi huu, lazima kwanza uache kuangalia matokeo ya haraka na kuangalia matokeo ya muda mrefu. Mara nyingi unapokazana na kupata matokeo ya haraka, unazuia makubwa ya muda mrefu. Lakini unapoachana na matokeo ya haraka, unatengeneza makubwa zaidi ya muda mrefu.

Fanya yako, ambayo ni kuweka kazi na iache dunia ifanye yake ambayo ni kukuletea wewe matokeo ya kazi yako. Usiingilie kazi zisizokuhusu, itakuwa kikwazo kwako kufanya sehemu yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha  

Normal
0

21

false
false
false

SW
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,sans-serif;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-language:EN-US;}