“No matter bow big mankind’s store of knowledge seems to me in comparison with our previous ignorance, it is only an infinitely small part of all possible knowledge.” – Leo Tolstoy
Haijalishi maarifa tuliyonayo sasa ni mengi kiasi gani,
Bado ni sehemu ndogo mno ya maarifa yanayoweza kupatikana.
Kadiri tunavyokwenda, maarifa yanaongezeka kwa kasi kubwa.
Kasi hii haitapungua, bali inazidi kukua kadiri teknolojia inavyokua.
Kwa kasi hii ya ongezeko la maarifa pia, unapaswa kujua huwezi kujua kila kitu. Huna muda wala nguvu za kuweza kujifunza maarifa yote yanayopatikana.
Kitu kingine muhimu cha kutambua ni kwamba maarifa mengi yanapingana.
Kwa kila utafiti unaosema A =2, kuna tafiti nyingine nyingi zinazopinga hilo.
Zenye ushahidi kabisa unaoonesha kinachodhaniwa ni sahihi siyo.
Tunahitaji kuwa na njia sahihi ya kukabiliana na mafuriko haya ya maarifa, ambayo yanaendelea kuwa makubwa kila siku.
👉🏽Kubali huwezi kujua kila kitu, badala ya kukimbizana na kujua kila kitu, badala ya kujiumiza kwa yale usiyojua, kubali kabisa kwamba huwezi kujua kila kitu.
👉🏽Usifike mahali na kuona tayari umeshajua kila kitu, utakuwa unajidanganya na utaanza kuanguka. Kila siku endelea kujifunza, haijalishi umepiga hatua kiasi gani
👉🏽Chagua yale maarifa yanayokuwezesha kupiga hatua. Tambua lengo lako kuu la kujifunza siyo kuwaonesha wengine unajua sana, bali kuweka kwenye matendo na kufanya mambo yako kwa ubora zaidi.
Kwa kuwa maarifa mengi yanapingana, chagua yale yanayokuwezesha kuwa bora zaidi kwenye kile unachofanya.
Tukizingatia haya, hatutapata taharuki kwa mafuriko ya maarifa yanayoendelea.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu thamani kuwa kubwa kuliko bei, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/23/2093
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.