“If you accomplish something good with hard work, the labor passes quickly, but the good endures; if you do something shameful in pursuit of pleasure, the pleasure passes quickly, but the same endures.” – Musonius Rufus
Kama ukikamilisha kitu kilicho sahihi kwa kuweka juhudi kubwa, maumivu ya kazi yanapita, lakini matokeo mazuri unadumu nayo kwa muda mrefu.
Kama ukikamilisha kitu kisicho sahihi ili kupata raha na starehe, raha hiyo hupita na maumivu utadumu nayo kwa muda mrefu.
Tambua kwamba hakuna namna unaweza kuyakimbia maumivu ya kazi au matokeo.
Unachoweza ni kuyasogeza mbele, na hapo unayafanya kuwa makubwa zaidi.
Chagua kuumia sasa ili baadaye matokeo yawe mazuri,
Kuliko kuchagua raha na starehe sasa na baadaye matokeo kuwa mabovu.
Weka kazi sasa, weka kazi mapema na hakuna kazi unayoweka ikapotea.
Unaweza usiyaone matokeo yake sasa, lakini baadaye yatakuwa wazi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kitu pekee wanachokijua maguru ambacho wewe hujui, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/25/2095
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.