“Most of what we say and do is not essential,” If you can eliminate it, you’ll have more time, and more tranquility. Ask yourself at every moment, ‘Is this necessary?’” – Marcus Aurelius
Mengi unayosema na kufanya siyo muhimu.
Na hayo ndiyo yanayomaliza muda wako, kukuchosha na kukuvuruga.
Kama utaweza kuacha mengi unayofanya sasa na ambayo siyo muhimu, utapata muda zaidi, nguvu zaidi na utulivu mkubwa.
Tunachoka sana kwa sababu tunahangaika na mengi yasiyokuwa na mchango wowote wa kutufikisha kule tunakokwenda.
Ni muhimu sana kulinda muda wako na nguvu zako kama unataka upige hatua kubwa.
Kuanzia sasa, kila unachoanza kukifanya, kabla hujaendelea jiulize swali hili, je hiki ndiyo kitu muhimu zaidi kwangu kufanya kwa sasa?
Jiulize swali hilo na ukishapata jibu lifanyie kazi.
Unapoianza siku yako, unapangilia yale muhimu kwako kufanya kwa siku hiyo.
Lakini kadiri siku inavyokwenda, kuna mengi muhimu yanajipenyeza, unahangaika nayo na yanakuchosha kwelikweli. Lakini mwisho wa siku, yanakuwa hayana mchango kwako kufika unakotaka kufika.
Kuepukana na hilo, usiendelee kufanya chochote kabla hujajiuliza kama ndiyo muhimu zaidi kwako kufanya.
Muda tulionao ni mfupi, nguvu tulizonazo zina ukomo na mambo ya kufanya ni mengi.
Usipokuwa na chujio zuri la kuchuja yale unayofanya, utahangaika sana na mwisho wa siku hutapiga hatua.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuanza kuishi vile unavyotaka sasa, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/12/2112
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.