“Every bird always knows where to make her nest. And if she knows how and where to make her nest, this means that she knows her purpose in life. And why does man, who is the wisest among all creatures, not know that which any bird knows, that is, his purpose in life?” —Chinese wisdom

Kila ndege anajua wapi eneo sahihi kujenga kiota chake.
Na pia anajua jinsi ya kukijenga kiota hicho kwa namna ambayo kitakuwa imara na salama kwake na makinda yake.
Kama kiumbe mdogo kama ndege anajua wapi na jinsi ya kujenga kiota chake, ina maana anajua kusudi la maisha yake.
Hakuna aliyemfundisha ndege huyo kuhusu kusudi, ni kitu ambacho tayari kipo ndani yake, ni yeye kukitakeleza.

Sasa inashangaa pale binadamu, mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kufanya maamuzi, anasema hajui kusudi la maisha yake.
Kwa akili zote na utashi ambao binadamu anao, anaweza kushindwa na ndege kwenye jambo la msingi kama kujua kusudi la maisha!
Haya yote yanatokana na mtu kutokujisikiliza yeye mwenyewe, kuhangaika na yake yanayofanywa na wengine, kufuata mkumbo.

Kusudi la maisha lina anzia ndani ya mtu, kwa mtu kuyaangalia mazingira yake na kisha kuona namna bora ya kukabiliana nayo.
Siyo kitu kilichoganda, bali ni kitu kinachotegemea eneo, wakati na mazingira.

Asubuhi ya leo tafakari ni lipi kusudi la maisha yako. Kama bado hujalijua kusudi hilo chukua hatua ya kulijua leo. Usikubali ndege wadogo ambao hapo ulipo umeshawasikia wameamka mapema na wanafanya yao, wakuzidi kwenye hilo.
Fanya zoezi hili rahisi, kila siku tenga dakika 60 za kukaa peke yako kwenye utulivu, usifanye chochote bali jisikilize tu. Acha mawazo yako yazurure yayakavyo, wewe yafuate tu.
Dakika 60 kila siku na haitachukua muda kuna vitu utaanza kuviona kuhusu maisha yako ambavyo hujawahi kuviona huko nyuma.
Haitakuchukua muda utalijua kusudi la maisha yako, na hapo utaweza kufanya makubwa.

Usikubali kuendelea na maisha ya mkumbo, maisha ambayo hata ndege hawezi kuyaishi.
Lijue kusudi la maisha yako na uliishi hilo, utapunguza sehemu kubwa ya changamoto zinazokukabili.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kujikana wewe mwenyewe, fungua hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/18/2118

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.