“Only in the storm can you see the art of the real sailor; only on the battlefield can you see the bravery of a soldier. The courage of a simple person can be seen in how he copes with the difficult and dangerous situations in life.” — Daniel Achinsky

Uimara wa nahodha unapimwa wakati bahari ikiwa imechafuka.
Uimara wa mwanajeshi unapimwa wakati wa vita.
Na uimara wako kwenye maisha unapimwa wakati unapitia magumu na changamoto mbalimbali.

Hivyo usilalamike wala kujaribu kuzikimbia changamoto mbalimbali unazokutana nazo kwenye maisha yako.
Badala yake zikabili, kwani unapozitatua unabaki ukiwa imara kuliko ulivyokuwa kabla ya changamoto hizo.

Asubuhi ya leo tafakari magumu na changamoto zote kubwa ambazo umewahi kupitia kwenye maisha yako.
Fikiria jinsi ulivyokuwa unazihofia wakati unakutana nazo, lakini baadaye zimekuacha ukiwa imara zaidi.
Labda ni kazi ulikosa au kufukuzwa na hilo likakuwezesha kuwa na biashara inayokuweka huru.
Huenda ni mahusiano yalivunjika na baadaye ukaweza kutengeneza mahusiano mengine bora zaidi.
Mifano ni mingi na kila mmoja kwenye maisha yake amewahi kupitia magumu na changamoto ambazo zimemuacha akiwa imara zaidi.

Hivyo usiogope wala kuzikimbia changamoto,
Badala yake kuwa imara zaidi na uzikabili changamoto zako.
Eneo muhimu unalopaswa kuliimarisha zaidi ni imani yako, maana hii ndiyo inapimwa zaidi wakati wa magumu na changamoto.
Unapokuwa na imani thabiti na unayoisimamia bila ya kutetereka, hakuna gumu lolote litakalokusumbua.
Kijenge kiimani, hiyo ndiyo silaha kuu ya kukabiliana na chochote kwenye maisha yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kubembelezwa na wateja, wakikuomba wanunue unachouza, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/27/2127

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.