“Don’t talk about your philosophy, embody it.” – Epictetus
Kusema ni rahisi na matendo ni magumu.
Huwa tunapenda kusema kuliko kutenda.
Lakini matendo yana sauti kubwa kuliko maneno.
Hivyo kama unataka kueleweka na wengine, usiwe tu mtu wa kusema kwa maneno, badala yake onesha kwa vitendo.
Chochote unachosimamia kwenye maisha au unachotaka watu waelewe, ukionesha kwa matendo watu wataelewa zaidi kuliko ukisema kwa maneno.
Hivyo kuwa mtu wa vitendo zaidi na maneno kidogo.
Kwenye zama tunazoishi sasa, zama ambazo kila mtu analimbilia kutoa maneno zaidi kuliko vitendo,
Zama za maonesho hasa kwenye mitandao ya kijamii,
Watu wameshajifunza kupuuza maneno,
Badala yake wanaangalia vitendo.
Ukiwa mtu wa vitendo, ukipeleka nguvu zako kwenye kufanya kilicho sahihi, utawafikia na kukubalika na wengi.
Asubuhi ya leo tafakari ni mara ngapi umekuwa unatumia nguvu kuwashawishi watu wakubali kitu fulani kuhusu wewe.
Labda ni falsafa au dini au tabia au msimamo mwingine wowote.
Hizo ni nguvu ambazo ulizipoteza bure, maana maneno tu hayawabadili watu.
Kuanzia sasa achana na maneno na kuwa mtu wa vitendo.
Chochote ambacho unataka watu waelewe kuhusu wewe,
Chochote unachotaka wakijue kwako,
Na chochote unachotaka kuwashawishi wengine,
Fanya kwa vitendo na siyo kusema kwa maneno.
Matendo yako yataoneokana na kueleweka haraka kuliko maneno.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu uimara wa madhaifu yako, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/30/2130
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante kocha kwa tafakari.
LikeLike