“You should abstain from arguments. They are very illogical ways to convince people. Opinions are like nails: the stronger you hit them, the deeper inside they go.” — Decimus Junius Juvenalis

Kama unafikiri unaweza kumbadilisha mtu kupitia kubishana, unajidanganya.
Unapobishana na mtu, anazidi kuamini kile anachosimamia.
Kadiri unavyomuonesha kwa nini hayupo sahihi, ndivyo anavyozidi kutafuta sababu za kuamini zaidi upande wake.

Kama huwezi kumbadili mtu kwa kubishana, zoezi zima la ubishani linakuwa ujinga na kupoteza muda.
Hivyo jiepushe sana na mabishano yoyote yale, hayana manufaa yoyote kwako na kwa unaobishana nao.
Watu wanaoutaka ukweli huwa wanajulikana na huwa wanakuja wakiwa tayari kujifunza na siyo kubishana.
Ukishaona mtu anatetea upande wake kwa gharama yoyote ile, usifikiri kumpa ukweli zaidi kutambadili, bali kutanfanya azidi kutetea upande wake.

Asubuhi ya leo tafakari ni mabishano mangapi umekuwa unashiriki siku za karibuni.
Iwe ni kuhusu dini, siasa, michezo, mapenzi na mengineyo.
Angalia ni nini kimebadilika kwako na kwa wale uliokuwa unabishana nao,
Hakuna kilichobadilika, zaidi ya kila upande kuzidi kuamini ndiyo uko sahihi zaidi.
Okoa muda wako na nguvu zako kwa kuepuka sana kila aina ya mabishano.
Mabishano hayajawahi kumshawishi au kumbadilisha mtu.
Kama unaamini uko upande sahihi, ishi kile unachosimamia na matokeo unayopata yataonekana na hayo yatawashawishi wengine waje kwako kujifunza na kuchukua hatua za kubadilika.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu ushindi hewa, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/03/2134

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.