“Do not be concerned too much with what will happen. Everything which happens will be good and useful for you.” — Epictetus
Mara nyingi umekuwa unahofia kuhusu mambo yanayoweza kutokea siku zijazo.
Hofu hizo zimekuwa zinakuzuia usichukue hatua ulizopanga kuchukua.
Na hilo linakuwa kikwazo kwa mafanikio yako.
Kitu muhimu unachopaswa kujua ni hiki;
Chochote kitakachotokea, kitakuwa na manufaa kwako.
Iwe kizuri au kibaya, unachotaka au usichotaka,
Kutakuwa na namna nzuri ya kutumia kila kinachotokea.
Hivyo usihofie tena chochote,
Badala yake chukua hatua sahihi,
Ukijua chochote kinachotokea, kitakuwa na manufaa kwako.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA tunaishi kwa MSINGI, MWONGOZO na MSIMAMO.
Kwa kufuata hayo wakati wote, hatuna wasiwasi wala hofu kuhusu matokeo tutakayopata,
Kwani tutaendelea kuongozwa na hayo.
Weka umakini wako kwenye kile unachofanya, yajayo yasikusumbue kwa namna yoyote ile.
Kwa sababu unajua chochote kinachokuja, utaweza kukitumia kwa manufaa kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kukubali kutokukubaliana, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/20/2151
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.