“Every habit and capability is confirmed and grows in its corresponding actions, walking by walking, and running by running… therefore, if you want to do something, make a habit of it.” – Epictetus

Kila tabia huwa inajengwa na kuimarishwa kwa vitendo, kupitia hatua ambazo mtu anachukua.
Kwa kujua hili, tunaweza kunufaika kwa njia mbili;

Njia ya kwanza ni kujenga tabia njema, kama kuna tabia unataka kujijengea, wewe jua ni hatua zipi unapaswa kuchukua kisha zichukue kila siku au mara kwa mara.
Kadiri unavyofanya ndivyo tabia inapata nguvu na kuwa imara.
Kwa tabia yoyote unayotaka kujenga, jua vitendo vya msingi kwenye tabia hiyo na vifanye.

Njia ya pili ni kuvunja tabia mbaya.
Kama una tabia mbaya na ambazo ni kikwazo kwako, kuzivunja unapaswa kuacha kufanya matendo ya tabia hizo.
Unapoacha kuitenda, inakosa nguvu na kufa.
Kwa kila tabia unayotaka kuivunja, angalia ni vitendo gani vya msingi kwenye tabis hiyo, kisha acha kuvifanya.
Tabia itakosa nguvu na kufa.

Kila kitendo unachofanya ni hatua ya kuimarisha tabia fulani.
Hivyo kabla hujafanya chochote, jiulize ni tabia gani unajenga au kuimarisha?
Kama ni tabia nzuri endelea, lakini kama ni tabia mbaya basi acha.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kufanya kama unatoa zawadi, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/24/2155

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.