“In the smithy the iron is softened by blowing up the fire, and taking the dross from the bar. As soon as it is purified, it is beaten and pressed, and becomes firm again by the addition of fresh water. The same thing happens to a man at the hands of his teacher.” – Johann Wolfgang von Goethe

Chuma kinapochimbwa, huwa siyo kisafi,
Hivyo hatua ya kwanza ambayo wahunzi hufanya ni kukisafisha.
Na hapo chuma kinapitishwa kwenye moto mkali kuondoa kila aina ya uchafu.
Moto mkali unaondoa kila takataka, lakini unakiacha chuma kikiwa kwenye hali ya kimiminika.
Hapo kinarudishwa kwenye hali yake ya ugumu kwa kupoozwa kwa maji.
Baada ya chuma kuwa safi, ndipo sasa kinatumika kutengeneza vitu mbalimbali, ambapo kitapondwa au kuyeyushwa tena ili kutengeneza kile kinachohitajika.
Mpaka kinakuja kutokea kifaa kizuri cha chuma na chenya matumizi, chuma hicho kinakuwa kimepitia magumu mengi.

Hivyo pia ndivyo inavyotokea kwa mtu anapokutana na mwalimu.
Karika kubadili maisha ya mtu, lazima apitie mchakato kama wa kufua chuma.
Lazima kwanza aondoe kila aina ya uchafu ambao amekuwa nao, tabia zisizo sahihi, kutokujifunza, uzembe, kutokujali na mengine.
Baada ya kila uchafu kuondoka, ndipo sasa anajengwa kuwa mtu mpya, kwa kujua nini anataka, gharama gani anapaswa kulipa na kuwa tayari kuilipa.

Mwalimu sahihi ni yule anayempitisha mwanafunzi wake kwenye hatua hizo bila ya kumuacha arudi nyuma.
Mwalimu anamsimamia na kumwongoza mpaka afike mwisho bila ya kumuonea huruma.
Kama mhunzi ataonea chuma huruma, haitakuwa safi na kutoa kitu chenye manufaa.
Kadhalika mwalimu akimuonea mwanafunzi huruma, mwanafunzi huyo hatakuwa bora.

Kila mmoja wetu ni mwanafunzi kwenye haya maisha, kuwa tayari kupitia magumu ili uwe bora zaidi ya ulivyo sasa.
Kadhalika kila mmoja wetu ni mwalimu kwa wengine, kuwa tayari kuwapitisha kwenye ugumu bila huruma ili wawe bora.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu bila namba unajidanganya, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/27/2158

Rafiki yako anayekupenda sana.
Kocha Dr Makirita Amani.