“Concentrate every minute like a Roman—like a man— on doing what’s in front of you with precise and genuine seriousness, tenderly, willingly, with justice.” – Marcus Aurelius

“Stick to what’s in front of you—idea, action, utterance.” — Marcus Aurelius

Mafanikio kwenye maisha hayatokani na yale unayofanya, bali yanayokana na jinsi unavyoyafanya mambo hayo.
Kama kufanya, kila mtu anafanya sana.
Kila siku watu wako bize kweli kweli,
Wanazimaliza siku wakiwa wamechoka kweli kweli,
Lakini angalia ni matokeo gani wamezalisha, hakuna kabisa.

Mafanikio hayatokani tu na kufanya, bali kufanya kilicho sahihi na kukifanya kwa umakini mkubwa sana.
Wengi wamekuwa wanafanya vitu juu juu, wanafanya kitu kimoja huku mawazo yao yako kwenye vitu vingine.
Matokeo yake wanazalisha matokeo ambayo siyo bora, kitu kinachowazuia wasifanikiwe.

Kila siku una mambo mengi ya kufanya kuliko muda ulionao,
Kila muda kuna watu wengine wanawinda umakini wako,
Na akili yako huwa ina tabia ya kuzurura hivyo, usipoidhibiti, unakosa umakini.

Chagua yale tu ambayo ni muhimu kwako kufanya na ukishachagua, yafanye kwa viwango vya juu mno.
Unapofanya kitu, umakini wako wote uende kwenye kitu hicho.
Mawazo yako yote yawe kwenye hicho unachofanya na ukifanye kwa umakini mkubwa mno.
Jiepushe na kila aina ya usumbufu ambao unakazana kunasa umakini wako.
Ukiweza kupata masaa mawili ya kufanya hivi, utakamilisha makubwa kuliko kutumia muda mwingi huku ukiwa na usumbufu na kukosa umakini.

Kwa zama tunazoishi sasa, umakini wako ndiyo mtaji wako.
Ulinde sana na utumie kwa yale makini pekee.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kutaka kuibadili dubia, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/28/2159

Rafiki yako anayekupenda sana.
Kocha Dr Makirita Amani.