Ndiyo vitu pekee vinavyoleta anguko kubwa baada ya mtu kuwa amefanikiwa.
Wote ambao waliwahi kufanikiwa na kufika ngazi za juu, lakini baadaye wakaanguka kutoka kwenye mafanikio yao, ni kwa sababu ya vitu hivyo viwili, kiburi na ujinga.
Kiburi ni pale mtu anapojua kitu sahihi anachopaswa kufanya, lakini hakifanyi. Mafanikio huwa yana tabia ya kujenga kiburi kwa wengi, kwa sababu wameshafanikiwa, hudhani wanaweza kupata kila wanachotaka hata kama hawatafuata mchakato sahihi. Hii huwapelekea watu kupuuza mambo ya msingi kabisa na hilo kuwapeleka kwenye anguko.
Ujinga ni pale mtu anapokuwa hajui na hivyo kufanya kitu kwa namna isiyo sahihi. Mafanikio yana tabia ya kuwafanya watu wasione ujinga wao na hivyo kujiamini kupita kiasi. Mtu anaweza kufanikiwa kwenye eneo moja, akafikiri anaweza kufanikiwa kwenye eneo jingine tofauti, kwa uzoefu aliopata kwenye eneo moja. Hapa ndipo ujinga unapopelekea wengi kuanguka. Kingine ni mtu kuona tayari ameshajua kila kitu na hahitaji tena kujifunza, hapo anabaki kwenye ujinga na kwenda kwenye anguko.
Kuondokana na hali hizi mbili, kuwa mnyenyekevu na tayari kujifunza kila wakati. Mafanikio yasikufanye unajua au kuweza zaidi, bali yakufanye uwe mtu wa kuendelea kujifunza na kufuata njia sahihi katika yote unayofanya. Hata kama umefanikiwa kiasi gani, kamwe usiisahau misingi iliyokufikisha kwenye mafanikio hayo, ukiikiuka, utaanguka. Kadhalika tambua huwezi kujua kila kitu, kuna mengi hujui hivyo kuwa tayari kujifunza kila wakati.
Mafanikio unayopigania hayapaswi kuwa andalio la kuanguka, epuka sana kiburi na ujinga ili udumu kwenye mafanikio yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante kocha sitakuwa na kiburi na ujinga nitakuwa mnyenyekevu kwa yale yanayonifanya niwe bora
LikeLike
Vizuri.
LikeLike