“I am an old man and have known a great many troubles, but most of them never happened.”
—MARK TWAIN
Kila ukiifikiria kesho yako, kuna mambo mengi yanakusumbua.
Yanakupa hofu na wasiwasi mkubwa.
Lakini leo hii ukichukua nafasi ya kujikumbusha mambo ambayo yamewahi kukusumbua huko nyuma, utagundua mengi hayakutokea kabisa.
Na hata kwa yale yaliyotokea, hayakuwa mabaya au magumu kama ulivyofikiria.
Hivyo kubwa la kujifunza hapa ni kwamba hupaswi kuhangaika na chochote ambacho bado hujakifikia.
Weka umakini wako kwenye yale yaliyo mbele yako sasa na yafanye kuwa bora zaidi.
Na jiweke tayari kukabiliana na lolote linaloweza kuja.
Ila kuhangaika na lipi litakuja, usipoteze muda wako kufanya hivyo.
Kwa sababu mengi hayatatokea na machache yatakayotokea, hayatakuwa kama unavyohofia sasa.
Binadamu ndiyo viumbe pekee ambao huwa tunajiumiza kwa mambo yaliyopita na ambayo hatujayafikia kabisa.
Ukifuta hali hizo mbili, utapunguza sana ugumu na mateso kwenye maisha yako.
Kuacha kusumbuka na yanayokuja haimaanishi uwe mzembe na kutokujali.
Badala yake inamaanisha uwe tayari kukabiliana na chochote, lakini ukabiliane nacho pale kinapokuja na siyo kwenye kufikiria kitakuja.
Vuka daraja pale unapolifikia, wakati mwingine, weka umakini wako kwenye safari na siyo kufikiria daraja ambalo bado hujalifikia litakuwaje.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu ukweli au hadithi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/02/2163
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.