“Just that you do the right thing. The rest doesn’t matter. Cold or warm. Tired or well-rested. Despised or honored. Dying…or busy with other assignments.” – Marcus Aurelius

Wajibu wako na kilicho muhimu kabisa kwako,
Ni kufanya kilicho sahihi.
Mara zote.
Haijalishi unapitia hali gani,
Haijalishi wengine wanafanya nini,
Wewe wajibu wako ni kufanya kilicho sahihi.
Ukishafanya kilicho sahihu,
Mengine yote yanakwenda sawa.

Na wajibu wako ni kufanya, siyi kuangalia matokeo gani unafanya.
Maana matokeo mazuri huwa yanachukua muda kuonekana,
Hivyo kama unasukumwa na matokeo tu, utakata tamaa haraka.

Iwe una njaa au umeshiba,
Umechoka au kupumzika,
Unaheshimika au kudharaulika,
Mara zote fanya kilicho sahihi.
Kwa kufanya kilicho sahihi, hakuna kitakachokuyumbisha.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu mtego wa mitandao ya kijamii kwenye umaarufu, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/07/2168

Rafiki yako anayekupenda sana.
Kocha Dr Makirita Amani.