“Do not live as if you have ten thousand years left. Your fate hangs over you. While you are still living, while you still exist on this Earth, strive to become a genuinely great person.” —Marcus Aurelius.

Unajua kabisa ya kwamba hutaishi milele,
Lakini jinsi unavyoyaendesha maisha yako na kutumia muda wako,
Utadhani umehakikishiwa miaka elfu moja mbele yako.

Kwa jinsi unavyopoteza muda na kuhangaika na yale yasiyo muhimu, ni kama vile unajua ni muda mrefu kiasi gani ulio nao hapa duniani.
Lakini hujui hilo, unabahatisha tu na hicho ndiyo kikwazo kikubwa.

Kila siku jikumbushe ya kwamba hutaishi milele,
Jikumbushe jinsi muda wako ulivyo mfupi, huku mambo ya kufanya yakiwa mengi.
Na hapo jiwekee vipaumbele sahihi,
Hangaika na yale tu yanayokufanya kuwa mtu bora, yanayokufikisha kwenye ukuu,
Mengine achana nayo maana hayana mchango kwako.

Muda uliona ni wa thamani kubwa mno, kwa sababu ukishapita hautarudi tena.
Upe muda huo thamani ambayo unastahili, kwa kuutumia kufanya yale ambayo yana mchango kwako kuwa bora na kuacha alama kubwa.

Usitawanye hivyo muda wako kama vile utaishi milele.
Kila unapofanya jambo la kupoteza muda, jikumbushe umejipunja kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu uwekezaji kwenye vitu muhimu, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/08/2169

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.