Tusingeweza kutembea duniani, maana tungekuwa tunateleza tu.

Tusingeweza kuanzisha moto.

Mashine zisingeweza kuwashwa wala kuzimwa.

Ndege zisingeweza kupaa angani.

Lakini ukinzani huo…

Unamaliza soli za viatu,

Unafanya vifaa vya mashine viishe haraka,

Unapelekea hitaji ya nishati kubwa kuendesha mashine mbalimbali.

Unaweza kuona jinsi asili inavyofanya kazi hapo, ukinzani unazuia vitu, lakini kuzuia huko kuna manufaa makubwa, na kuna gharama pia ya kuvuka ili ukinzani huo.

Hivyo pia ndivyo maisha yalivyo, bila ya ukinzani hakuna maisha, bila ya ukinzani hakuna maendeleo na mafanikio.

Hivyo unapokutana na ukinzani wowote, jua hiyo ndiyo njia ya kufikia kile unachotaka, jua kuvuka ukinzani huo kutakupa matokeo makubwa.

Usikimbie chochote kinachosimama kati yako na kile unachotaka, bali kikabili. Kama ambavyo ndege haiwezi kuruka kwa sababu kuna ukinzani wa hewa, lakini inapowashwa inakuwa na nguvu ya kuvuka ukinzani uliopo.

Ukinzani ni nguvu, ambayo inahitaji nguvu kubwa zaidi kuuvuka.

Kwa kila ukinzani unaokutana nao, angalia ni nguvu kubwa zaidi ipi unayopaswa kuweka ili kuvuka ukinzani huo, na kuwa tayari kuivuka ili uweze kupata kile unachotaka.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha