“Do not believe in words, yours or others’; believe in the deeds.” – Leo Tolstoy

Kusema ni rahisi,
Kupanga ni rahisi,
Lakini kuchukua hatua kwenye yale ambayo mtu anasema na kupanga siyo rahisi.
Hivyo unachopaswa kuamini kwako mwenyewe na hata kwa wengine siyo maneno, bali matendo.

Usidanganyike na kile watu wanasema, bali angalia kile wanachofanya.
Wanachosema au kupanga ni matarajio yao,
Wanachofanya ni uhalisia wao.
Hivyo kama unataka kuujua ukweli, angalia matendo na siyo maneno.

Kuna watu ni wazuri sana kwenye maneno, wana ushawishi mkubwa, ukiwasikiliza tu unawaamini moja kwa moja.
Epuka sana hilo, usikimbilie kumwamini mtu haraka kabla hujayaona matendo yake.
Wengi wanaoongea sana huwa siyo watendaji.

Na kwako binafsi, punguza maneno na ongeza matendo.
Matendo yanasema kwa nguvu na kuaminika kuliko maneno.
Hivyo kama unataka kuwashawishi watu, fanya hivyo kwa matendo na siyo maneno.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kwa sababu hawawezi kuishi bila hivyo, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/12/2173

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.