“You have to set goals that are almost out of reach. If you set a goal that is attainable without much work or thought, you are stuck with something below your true talent and potential.” — Steve Garvey

Malengo yoyote unayojiwekea, yanapaswa kuwa zaidi ya uwezo wako.
Iwe ni kitu ambacho hujawahi kukifanya au kukifikia.
Kwa namna hiyo utajisukuma zaidi na hata kama hutayafikia, utapata zaidi ya ulivyozoea kupata.

Kinachowakwamisha wengi na kuwazuia kufikia uwezo mkubwa ulio ndani yao ni kuweka malengo ambayo yako ndani ya uwezo wao wa kuyafikia, ambayo walishayafikia huko nyuma.
Kwa kuweka malengo ya aina hiyo, mtu hawezi kujua uwezo mkubwa ulio ndani yake.

Njia pekee ya kujua unaweza kwenda mbali kiasi gani ni kwenda mbali zaidi ya ulivyozoea.
Njia pekee ya kujua unaweza kufanya makubwa kiasi gani ni kufanya makubwa kuliko ilivyozoea.

Hivyo kwa chochote unachotaka kufanya, weka malengo na mipango mikubwa kuliko ulivyozoea, kisha jisukume kufikia.
Ni katika kujisukuma huko ndiyo utaweza kujua uwezo mkubwa ulio ndani yako.

Kwa chochote ambacho umewahi kufanya,
Kwa popote ambapo umefika,
Jua unaweza kwenda zaidi ya hapo.
Anza kwa kuweka malengo na mipango mikubwa kuliko mazoea na utaweza kwenda zaidi ya pale ulipo sasa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu sababu ya kufanya kazi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/18/2179

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.