“What’s thrown on top of the conflagration is absorbed, consumed by it—and makes it burn still higher.” – Marcus Aurelius

Moto mkubwa na unaowaka kwa ukali, huwa unageuza kila kinachowekwa kwenye moto huo kuwa nishati na kuwaka zaidi.
Moto huo hauogopi chochote unachopokea, badala yake unakipokea na kukigeuza moto unaowaka zaidi.

Yageuze maisha yako kuwa kama moto wa aina hiyo,
Moto unaowaka kuelekea kwenye ndoto yako,
Na chochote kinachotupwa kwenye maisha yako, unakigeuza kuwa nishati ya kufikia ndoto yako.

Hata pale watu wanapojaribu kukurudisha nyuma na kukukatisha tamaa, unageuza hiyo kuwa hamasa ya kupiga hatua zaidi.

Wafanye watu wastaajabu kwa namna unavyotumia kila unachokutana nacho kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
Ukiweza hilo, hakuna kinachoweza kuwa kikwazo kwako kufikia ndoto yako.

Inapokuja kwenye ndoto yako, yafanye maisha yako kuwa moto mkubwa, ambao unameza kila kinachoingia kwenye moto huo na kuwasha moto zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kama umeridhika inatosha, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/19/2180

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.